• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TARURA yajenga daraja lenye thamani ya sh.bilioni 1.6 Tunduru

Imewekwa kuanzia tarehe: August 26th, 2022

WAKALA wa barabara mijini na vijijini(Tarura) wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,umekamilisha ujenzi wa daraja  kubwa na la kisasa linalounganisha kijiji cha Fundimbanga,Matemanga na maeneo mengine ya wilaya ya Tunduru.

Meneja wa Tarura wilaya ya Tunduru Silvanus Ngonyani alisema,daraja la Fundimbanga limejengwa katika awamu kuu mbili na pamoja na barabara zake limeigharimu serikali jumla ya Sh.bilioni 1.456  na limekamilika kwa asilimia mia moja  na limeanza kutumiwa na wananchi kwa ajili ya shughuli zao maendeleo.

Alisema,daraja hilo lina urefu wa mita arobaini na tano na upana wa mita nane na vivuko vya watembea kwa miguu kushoto na kulia  mita moja moja na lina uwezo wa kubeba magari yenye uzito wa zaidi ya tani ishirini.

Alielezwa kuwa,kukamilika kwa daraja hilo kumemaliza kabisa changamoto ya madereva wa vyombo vya moto na wananchi kupoteza maisha kwa kutumbukia katika mto Nanyungu kipindi cha masika.

Ngonyani alisema,serikali kupitia wakala wa barabara mjini na vijijini(Tarura) inaendelea kutekeleza na kujenga miradi mbalimbali katika wilaya hiyo ili kuwezesha wananchi kusafiri na kusafirisha bidhaa na mazao yao kwa urahisi katika kipindi chote cha mwaka.

Amewaomba wananchi,kulitunza daraja hilo na miundombinu yake ili liweze kudumu kwa muda mrefu na kuleta tija iliyousudiwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Wananchi wa kijiji cha Matemanga,Fundimbanga  na Ligunga vinavyounda tarafa ya Matemanga,wameishukuru Serikali kukamilisha ujenzi wa daraja hilo ambalo awali  kulikuwa na daraja la miti, jambo lililohatarisha  usalama wao na kurudisha  nyuma uchumi wao.

Adam Omari mkazi wa Fundimbanga alisema,nyakati  za masika maji yalifunika daraja hilo la miti hatua ambayo ilisababisha  baadhi ya wananchi na vyombo vya moto kusombwa na maji na wengine kupoteza maisha.Aidha alisema, hata wanafunzi wanaosoma shule ya Sekondari Matemanga wanaoishi kijiji cha  Fundimbanga walilazimika kuzunguka umbali mrefu wakikwepa  eneo hilo hatarishi.Luka Luoga alisema kabla ya Tarura kujenga daraja, eneo hilo  halikuweza kupitika kiurahisi, hivyo wananchi wa Fundimbanga na Matemanga walishindwa kusafirisha mazao yao kwenda sokoni na hivyo kutoa nafasi kwa walanguzi kwenda kununua mazao kwa bei ndogo.

Aliongeza kuwa,lakini  baada ya kukamilika kwa  ujenzi huo eneo hilo linapita kipindi chote cha mwaka bila usumbufu na kuipongeza Serikali kwa kazi nzuri ya kuboresha miundombinu ya barabara.

Naye Issa Lukoko mkazi wa Ligunga alisema,kujengwa kwa daraja  hilo kumefungua mawasiliano katika kijiji cha Fundimbanga na tarafa  yote ya Matemanga  na kumechangia kasi ya  ukuaji wa biashara kwa kuwa wakulima wengi wanapita katika daraja hilo kupeleka mazao yao mjini kwa ajili ya kutafuta masoko.

Alisema,katika kijiji cha Fundimbanga changamoto kubwa na ya muda mrefu ilikuwa kukosekana kwa daraja katika mto Nanyungu na walikuwa wakipata wakati mgumu kipindi cha masika hasa wanafunzi kuvuka kwenda upande wa pili,hali iliyopelekea wengine kuacha masomo ambapo ameipongeza Tarura kujenga daraja la kudumu.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.