• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TARURA yatumia milioni 629 kujenga daraja jipya Tunduru

Imewekwa kuanzia tarehe: May 22nd, 2023

SERIKALI kupitia wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA imetumia kiasi cha Sh.milioni 629 kujenga daraja jipya katika mto Nanjoka linalounganisha kata ya Nakayaya na Majengo wilayani Tunduru.

Ujenzi wa daraja hilo,unatokana na daraja la zamani kusombwa na maji kufuatia mvua  kubwa zilizonyesha mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu ambazo zilileta maafa makubwa kwa wananchi na kuharibu miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Meneja wa TARURA wilayani Tunduru Mhandisi Silvanus Ngonyani amesema,  hadi sasa ujenzi wa daraja hilo umefikia asilimia 98.5 na limeanza kupitika.

Amesema,daraja la Nanjoka lilitakiwa kujengwa kwa muda wa miezi mitano,hata hivyo kutokana na jitihada za Tarura na uwezo wa mkandarasi kazi imekamilika katika kipindi kifupi.

Ngonyani ametaja kazi zilizobaki ni ujenzi wa mifereji upande wa kulia na kushoto urefu wa mita 300 na kuendelea kufukia mashimo sehemu chache  kwa ajili ya kuimarisha daraja na barabara.

Ngonyani, amewataka wananchi kuzingatia sheria za utunzaji wa mazingira kwa kutofanya shughuli za binadamu ndani ya mita 30 kuanzia katikati ya mto ili kutoathiri miundombinu ya barabara zinazojengwa kwa fedha nyingi.

Kwa mujibu wa Ngonyani,kutozingatia sheria ya mazingira ndiyo sababu iliyopelekea hata daraja la awali kusombwa na maji kwani baadhi ya wananchi walitumia vibaya sehemu ya juu ya mto kufanya shughuli za kibidamu ikiwemo kilimo na ufugaji wa samaki jambo lililosababisha  mto Nanjoka kupanuka.

“Tunduru tuna tatizo kidogo la wananchi kugeuza mifereji inayopitisha maji kuwa sehemu ya madampo,tunawaomba wananchi kuzingatia sheria za mazingira na kutunza barabara zinazojengwa kwa manufaa yao”alisema Ngonyani.

Alisema,kukamilika kwa daraja hilo la kisasa kunatoa fursa kwa wananchi kusafiri na kusafirisha mazao kutoka shambani kwenda sokoni na kusisitiza kuwa,ni muhimu kwa jamii kuhakikisha inatunza miudombinu inayojengwa kwa gharama kubwa.

Mkazi wa mtaa wa Majengo Saleh Haji,ameishukuru Serikali kujenga daraja la kudumu katika eneo hilo baada ya daraja la awali kusombwa na maji na kuleta adha kubwa kwao na kushindwa kuvuka kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Alisema,daraja jipya ni bora tofauti na la zamani kutokana na kujengwa kwa viwango vikubwa hasa  maeneo ya kupitishia maji chini ya daraja na kuwapongeza wasimamizi wa ujenzi huo wakala wa barabara za mijini na vijijini Tarura kwa kazi nzuri.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.