Mfuko wa kunusuru kaya masikini Nchini (TASAF) imepanga kuzifikia kaya masikini milioni 1.45 sawa naongezeko la kaya laki tatu kwa kipndi cha pili awamu ya tatu.
Hayo ameyasema Gerson Mboramallamia kwaniaba ya Mkurugenzi wa TASAF Nchini kwenye kikao cha kuwajengea uwezo viongozi,watendaji na wawezeshaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini kipindi cha pili awamu ya tatu kilicho fanyika katika ukumbi wa SACCOS ya Walimu Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Mboramallamia amesema azma ya Serikali kupitia TASAF ni kupunguza umasikini wa kipato na kuongeza kipato kwenye kaya masikini kwa kutumia rasilimali zilizopo kwa kuboresha huduma za jamii kama vile huduma ya maji , afya, barabara na vivuko kwa walengwa kufanyakazi.
Amesema katika awamu ya kwanza ya utekelezaji TASAF imefanikiwa kupunguza umasikini wa kaya kwa asilimia 10 na umasikini uliokithiri kwa asilimia 12 kwa walengwa kufanya shughuli za kiuchumi za ufugaji,kilimo,uvuvi,biashara ndogondogo na ajira za muda mfupi.
Ameongeza kwa kusema TASAF kipindi cha awamu ya kwanza kiliwafikia walengwa kwa asilimia 70 na kipindi hiki cha pili awamu ya tatu kimepanga kukamilisha asilimia 30 iliyobaki na kufikisha asilimia miamoja ya walengwa wote Nchini iliwaweze kunufaika na mfuko huo kupitia ruzuku za aina nne ambazo mfuko umebanisha katika kukabiliana na tatizo la umasikini
Mboramallamia amezitaja aina za ruzuku zitakazo tolewa kuwa ni ruzuku ya msingi inayotolewa kwenye kaya iliyopo kwenye mpango,ruzuku ya kutimiza masharti inayotolewa kwa kaya yenye walengwa wanaotakiwa kutimiza masharti ya elimu na afya ,ruzuku ya walemavu inayotolewa kwa walemavu na ruzuku ya Watoto inayotolewa kwa Watoto wanaoishi kwenye kaya masikini.
Kwaupande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Pendo Daniel ameomba TASAF makao mkuu kuwarejesha kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini walengwa ambao waliondolewa kwenye mpango baada ya kufanyika kwa uhakiki wakuzitambua kaya zinazostahili kuwepo kwenye mpango.
“Nimefurahishwa sana na maboresho ya kipindi hiki cha pili awamu ya tatu kwakufanya uhakiki na kuwabaini walengwa hewa ambao hawakustahili kuwepo kwenye mpango”,amesema Mhe.Menas Komba
Mhe. Komba amesema TASAF licha ya kunusuru kaya masikini imesaidia sana kaya hizo kujiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa ambayo inamwezesha mlengwa na wategemezi wake watano kupata huduma za matibabu kwa gharama ya shilingi elfu 30,000 kwakipindi cha mwaka mmoja.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Simoni Bulenganija amewataka watendaji ambao wameteuliwa kufanya zoezi la uhakiki awamu hii kwenda kufanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa na kuzingatia kiapo walichoapa.
Bulenganija amesema katika eneo la usimamizi na ufuatiliaji amejipanga vema katika zoezi hilo ili kuhakikisha kazi ya kuibua kaya masikini zenyesifa linafanikiwa kama Serikali inavyokusudia kufanikisha mpango wake wa kunusuru kaya masikini na umasikini uliokithiri nchini.
Mratibu wa TASAF wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Hosana Ngunge amesema katika zoezi la utambuzi wa kaya masikini jumla ya wataalam tisa wameteuliwa kutekeleza kazi hiyo katika Vijiji 24 ambavyo awali havikuwaepo katika mpango.
Halmashauri ya wilaya ya Songea inajumla ya kaya 2743,Vijiji 56 ambavyo vyote vinaingizwa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini wa kipindi cha pili awamu ya tatu.
Mpango wa TASAF kipindi cha pili awamu ya tatu kilizinduliwa na hayati Rais Dkt John Pombe Magufuli mwaka 2020 na mpango huo utakamilika mwaka 2023.
Imeandikwa na Jacquelen Clavery
Afisa Habari Songea
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.