SERIKALI kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii nchini (TASAF), imetoa zaidi ya shilingi milioni 395 kutekeleza miradi 6 katika vijiji vya Parangu na Mdunduwalo katika Halmashauri ya wilaya Songea.
Akizungumza kwenye mkutano huo mbele ya uongozi wa Halmashauri pamoja na Wananchi Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Pendo Ndumbaro, alisema kukamilika kwa miradi hiyo italeta tija kwao kwani itawawezesha wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini na jamii kufanya biashara za uhakika na hivyo ni jukumu lao kushiriki hatua zote za ujenzi wa miradi hiyo
Alisema,kati ya Fedha hizo, kijiji cha Parangu kimepokea shilingi milioni 225 za ujenzi wa miradi mitatu ambapo ni standi, uwekaji wa vigaya pamoja na kujenga matundu manne ya vyoo na uzio.
Aidha,kijiji cha Mdunduwalo kimepokea shilingi milioni 170 za ujenzi wa miradi mitatu ujenzi wa nyumba ya madaktari wawili, matundu sita ya vyoo pamoja na uchimbaji wa kisima kirefu cha maji.
“Ni matumaini yangu miradi hii itakuza uchumi wa kaya pamoja na kuongezeka kwa kipato cha mtu mmoja mmoja pia kujengwa kwa miradi hii 6 katika vijiji vya Parangu na Mdunduwalo itaongeza upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii”alisema Daniel.
Hata hivyo, amewasisitiza viongozi wa vijiji pamoja na kamati za ujenzi wa miradi hiyo kushirikiana na wananchi katika kutekeleza ujenzi kwani asilimia 10 ya ujenzi itatolewa na wananchi katika kufanikisha kukamlikia kwa miradi yote
Kwa upande wake Mwenyekeiti wa Halmashauri hiyo Menasi Komba,amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kwa uamuzi wake wa kutoa fedha hizo za miradi ambazo zitatumika kujenga miradi hiyo na kuwaomba wananchi wailinde mradi hiyo nakushiriki hatua zote za ujenzi
“Wale wote watakaobainika kuiba zivifaa vya ujenzi kwenye miradi hii hatua zitachukuliwa haraka, pia niwaombe wajumbe na wanakamati wa miradi wa vijiji vyote viwili msishawishike hizi fedha zimeletwa kwa malengo ya kukuza uchumu wa kaya zetu”alisema Komba.Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wenzake Nicodemus Nyoni mkazi wa kijiji cha Parangu, amemshukuru Mbunge wa jimbo hilo Jenista Mhagama kwa kuweza kupeleka fedha za miradi wa ujenzi wa stendi ambapo itakapokamilika itawasaidia kujipatia kipato na kuwa na uhakika wa kupata huduma mbalimbali.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.