• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TASNIA ya habari imevamiwa-RC Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: February 4th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas  amesema tasnia ya Habari ni miongoni mwa tasnia zilizovamiwa na  baadhi ya watu ambao hawana sifa hali inayosababisha kuididimiza tasnia hiyo yenye mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi.

Kanali Thomas ameyasema hayo mjini Songea, baada ya kusikiliza kero,maoni na mapendekezo ya wanahabari wa Mkoa wa Ruvuma ikiwa ni ratiba yake inayoendelea na kukutana na makundi mbalimbali kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

“Kuendelea kuwa na wanahabari wasiokuwa na sifa ni kuididimiza tasnia,leo hii serikali inatangaza ajira kwa wanahabari zikiwemo za maafisa Habari,kama una elimu ya cheti huwezi kuajiriwa,kama una cheti nenda kasome upate diploma na degree ,unaweza kujiunga na Chuo Kikuu Huria, unafanya kazi zako huku unaendelea na chuo’’,alisisitiza.

Amesisitiza kuwa taaluma ya Habari inabadilika kila siku hivyo ili kuendena na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ya habari na mawasiliano  ni lazima wanahabari kujiendeleza kielimu.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amewataka wanahabari wanapoandika Habari kuzingatia usalama wa Mkoa na Taifa  ambapo amewakumbusha  kuandika Habari kwa kuzingatia sheria na maadili ya uandishi wa habari.

Amekemea baadhi ya tabia ya wanahabari kutishia watendaji kuwaandika vibaya,pale wanaposhindwa kuwawezesha ambapo amesema kufanya hivyo ni kinyume cha maadili ya kazi.

Mkuu wa Mkoa amewataka wanahabari kujenga mahusiano na wakuu wa Taasisi za serikali na binafsi na kwamba wasitumike vibaya kwa maslahi binafsi badala yake kalamu zao zitumike kwa maslahi ya Taifa.

Hata hivyo amewataka wanahabari kupigania haki zao kama wanavyopigania haki za watu wengine na kwamba ameahidi changamoto na mapendekezo waliyoyatoa atayafanyia kazi ili waweze kufanya kazi kwa tija na ufanisi .

Awali wanahabari walizitaja changamoto mbalimbali zinazowakabili kuwa ni zaidi ya asilimia 95 ya wanahabari mkoani Ruvuma hawajaajiriwa badala yake wanafanya kazi kama vibarua hivyo kutekeleza majukumu yako kwenye mazingira magumu.

Wameomba kuwe na mzunguko wa wanahabari kwenye ziara za kimkoa na kitaifa badala ya kutumia waandishi wachache ili kila Mwandishi aweze kunufaika na ziara hizo.

Waandishi wameomba maafisa Habari kuwa kiungo kwa waandishi na watendaji wa serikali katika ngazi za Halmashauri na Taasisi za serikali ili viongozi hao waweze kufikika kwa urahisi.

Licha ya changamoto hizo waandishi wa Habari wameipongeza serikali mkoani Ruvuma kwa kusimamia vema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo  katika sekta za kilimo, afya, elimu,maji,miundombinu na sekta nyingine ambayo inaendelea kuwanufaisha wananchi.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.