Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema tasnia ya habari mkoani Ruvuma imempoteza mtu muhimu baada ya kifo cha mwanahabari mkongwe Adamu Nindi aliyekuwa Mwakilishi wa Kampuni ya Sahara Media mkoani Ruvuma .
Kanali Abbas amesema hayo wakati anazungumza kwenye maziko ya mwandishi huyo yaliyofanyika kwenye makaburi ya Mjimwema mjini Songea
Marehemu Adamu Nindi ambaye alizaliwa mwaka 1954 katika kijiji cha Chiulu Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma amefariki Aprili 4 mwaka huu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa (HOMSO) mjini Songea.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.