• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TATHIMINI ukusanyaji mapato kuwezesha Halmashauri nchini kujitegemea

Imewekwa kuanzia tarehe: January 14th, 2023

MKURUGENZI wa Sera na Mipango Ofisi ya Rais TAMISEMI John Mihayo Cheyo amesema ofisi yake inafanya zoezi la tathimini ya ukusanyaji wa mapato katika Halmashuri zote 184 Tanzania Bara.

Amesema zoezi hilo limeanza Januari 9 mwaka huu na linafanyika kwenye Halmashauri na mikoa yote Tanzania bara na kwamba zoezi hilo linajumuisha wataalam kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA,Wizara ya Fedha,Ofisi ya Mkoa husika na Halmashauri zake.

Akizungumza katika mahojiano maalum Mkoani Ruvuma,Mkurugenzi huyo wa Sera na Mipango amesema kwa ujumla wakurugenzi wa Halmashauri nchini kote wamefurahia zoezi la tathimini  ya ukusanyaji wa mapato na wameshauri liwe zoezi endelevu.

“Zoezi hili la tathmini ya ukusanyaji mapato ambalo linafanyika nchi nzima linaweza kutuongezea mapato mengi kwenye Halmashauri na hatimaye kuzifanya Halmashauri zetu kuanza kujitegemea’’, alisisitiza Cheyo.

Hata hivyo amesema kukamilika kwa zoezi hilo kutawezesha kufanya makisio  ya mapato ya uhalisia katika Halmashauri kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024.

Mkurugenzi huyo anawapongeza  viongozi wote wa TAMISEMI kuanzia Katibu wa TAMISEMI,Kamishina Mkuu wa TRA na makatibu tawala wa mikoa yote nchini kwa kusimamia kikamilifu zoezi la tathimini ya ukusanyaji mapato.

Kwa upande wake Mchumi Ofisi ya Rais TAMISEMI Flugence Matemele  ambaye alikuwa kiongozi wa Timu ya  Tathimini ya kusanyaji mapato ya ndani kwenye Halmashauri mkoani Ruvuma,amesema zoezi limekwenda vizuri na wakurugenzi wa Halmashauri wametoa ushirikiano wa kutosha.

Amesema katika tathimini hiyo wamefanikiwa kuchambua chanzo cha mapato kimoja kimoja kwa kila Halmashauri kuanzia vyanzo vikubwa wanavyovigemea ambavyo vimebainika vinachangia mapato kuanzia asilimia 22 hadi 58.

Matemele amesema wakati wanafanya uchambuzi huo wamebaini kuna uwekezekano mkubwa wa vyanzo hivyo vya mapato kukusanya mapato mengi zaidi kama vitasimamiwa kwa nguvu zaidi.

“Wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wao   wamethibitisha bado walikuwa wanafanya makisio ya bajeti ya kukusanya vyanzo vya mapato kwa kutumia ozoefu tu,lakini katika tathimini hii tumewasisitiza kutumia takwimu’’,alisema Mchumi wa TAMISEMI.

Hata hivyo  ameitaja changamoto ambayo imeonekana kwenye tathimini hiyo kuwa ni wataalam kufanya makisio bila kuzingatia takwimu ambapo wataalam hao wameahidi kuanzia sasa watafanya makisio yenye uhalisia.

Amesema zoezi hilo la tathimini ya kusanyaji mapato limeiungaisha TAMISEMI na Taasisi muhimu kama TRA ili kushirikiana na Halmashauri  katika uboreshaji ukusanyaji mapato ya ndani katika Halmashauri zote nchini.

Naye Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Henry Kaiwanga  amesema katika tathimini ya ukusanyaji mapato walioufanya katika Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma wamebaini kuwa vyanzo vikuu vya mapato ni mazao ya kilimo,misitu na madini ambapo wamebaini makusanyo yanayokusanywa ni kiwango kidogo sana kutokana na makadirio ya chini.

Hata hivyo amesema wamebaini changamoto ya  tofauti ya takwimu kwenye ukusanyaji mapato kati ya TRA na Halmashauri husika ambapo imebainika Halmashauri ina takwimu zake na TRA ina takwimu zake hali inayochangia makusanyo hafifu.
Amesema kutokana na tathmini hiyo wameshauri maafisa mapato wa TRA na maafisa wa Halmashauri kufanya kazi kwa Pamoja ili Taasisi zote  mbili zikusanye mapato zaidi.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Jumanne Mwankoo  ameipongeza Ofisi ya Rais TAMISEMI  kwa kufanya zoezi hilo ambalo limekuwa na umuhimu mkubwa katika kuboresha mapato ya ndani katika Halmashauri zote nchini.

Amesema zoezi hilo limeongeza uelewa kuhusu makisio ya mapato ya ndani kwenye Halmashauri kwa sababu wataalam walikuwa wanafanya makisio kwa mazoea.

 Hata hivyo uchumi wa Mkoa wa Ruvuma umeendelea kuimarika kwa kuchangia asilimia 3.8 ya pato la Taifa ukiwa juu ya mikoa mingine ya Kanda ya Kusini Mashariki.

Kwa mujibu wa Takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu,Pato la Taifa (GDP) la Mkoa wa Ruvuma liliendelea kuongezeka kutoka shilingi bilioni 3.147 mwaka 2014 hadi kufikia shilingi bilioni 6.106 mwaka 2021.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Januari 14,2023

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.