• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TAWA Ruvuma wakamata meno ya tembo

Imewekwa kuanzia tarehe: May 18th, 2022

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma kwa kushirikiana  na Jeshi la Uhifadhi Wanyamapori (Tawa) kanda ya kusini, limewakamata watu watatu wakazi wa wilaya ya Tunduru wakiwa na meno tisa na  vipande vinane vya meno ya Tembo.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishina msaidizi Joseph Konyo aliwataja watu hao kuwa ni Said Awadi,Hassan Hakimu na Zakaria Rashid  na walikamatwa tarehe 10 Mei 2022 majira ya saa mbili usiku katika kijiji cha Milonde-Kiuma.

Kamanda Konyo alisema,meno  hayo yana uzito wa kg 20.4 na thamani yake ni Sh. milioni 138,600,000 ambapo watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika.

Aidha Konyo alisema,Jeshi la Polisi na askari wa Tawa wamefanikiwa kukamata  meno Matano ya Tembo yenye uzito wa kg 44 yenye thamani ya Sh.103,950,000.

Alisema,meno hayo yalikamatwa katika kijiji cha Hanga- Monastery wilayani Namtumbo, baada ya kutelekezwa na watu ambao walistukia mtego uliowekwa na Polisi na askari wa Jeshi la Uhifadhi,hata hivyo jitihada za kuwatafuta na kuwakamata  zinaendelea.

Kwa mujibu wa Kamanda Konyo,jumla ya Tembo saba waliuawa katika matukio hayo mawili na kila tembo mmoja ana thamani ya Dola za  Kimarekani  1,500 sawa na pesa za Kitanzania  Sh.milioni 242,550,000 kwa Tembo wote.

Alisema,kupatikana kwa nyara hizo na kukamatwa kwa watu hao kunatokana na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Jeshi la Polisi na Jeshi la Uhifadhi Wanyamapori(Tawa).

Kwa upande wake Kamishina msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Uhifadhi Wanyamapori(Tawa)kanda ya kusini Abraham Jullu,amewataka wananchi kuepuka vitendo vya uwindaji haramu wa wanyamapori wakiwamo Tembo ambao ni rasilimali na tunu kubwa za Taifa.

Alisema,uvunaji(uwindaji) haramu wanyamapori ni kosa kisheria kwani wanyama hao wanalindwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kuvutia  wageni na Watanzania wanaokwenda kutembelea Hifadhi za Taifa na kutoa fedha ambazo zinazochangia kukuza uchumi wa nchi yetu.

Alisema,Tawa na  vyombo vingine vya ulinzi na usalama vitahakikisha inawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakojihusisha na vitendo vya uwindaji haramu.

Kamishina Jullu, ameitaka jamii kusaidiana na mamlaka husika kulinda rasilimali zilizopo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho,badala ya kutanguliza maslahi binafsi.

Katika hatua nyingine Kamanda Konyo alieleza kuwa,kuanzia tarehe 1 hadi 12 Mwezi huu Jeshi hilo limefanya operesheni maalum iliyolenga kuwakamata watu wanaojihusisha na matukio ya uvunjaji,wizi na wapokeaji wa mali za wizi katika  maeneo mbalimbali.

Kamanda Konyo alisema,katika operesheni hiyo wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa kumi na sita kati yao wanaume kumi na tatu  na wanawake watatu wakiwa na vitu vya wizi.

Alitaja vitu vilivyokamatwa ni Televisheni kumi,Radio Subwofer nne,spika moja,magodoro mawili,mitungi mitano ya Gesi,viti vya Plastiki kumi,ndoo hamsini za mafuta ya kula,kitanda,mabegi ya nguo na baiskeli moja.

Ametoa onyo kwa watu wanaojihusisha na shughuli za ujangili na matukio ya wizi kuacha mara moja, kwani Jeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama havitawafumbia macho.

Imeandikwa na Albano Midelo

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Mei 17,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.