• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TFS waagizwa kuongeza kasi ya kupanda miti

Imewekwa kuanzia tarehe: February 23rd, 2022

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge,ameagiza wakala wa huduma za Misitu Tanzania(TFS)kutumia mvua zinazoendelea kunyesha, kuongeza kasi ya kupanda miti katika maeneo ya wazi yaliyoathiriwa na shughuli za kibinadamu katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Ibuge ametoa agizo hilo jana, wakati akizundua mpango wa upandaji miti kimkoa uliofanyika katika kijiji cha Mwande kata ya Mateteleka Halmashauri ya Madaba wilayani Songea.

Aidha Brigedia Ibuge,amewaonya wananchi kuacha tabia mbaya ya kuchoma kwa makusudi miti inayopandwa na Serikali kupitia wakala wa huduma za misitu(TFS)kwa kuwa hiyo ni sehemu ya miradi inayoliingizia Taifa fedha nyingi.

Alisema,kuchoma moto kwa makusudi mashamba ya miti ni ushamba na kamwe Serikali haitawavumilia hata kidogo watu hao kwa sababu Serikali inatumia fedha nyingi kuandaa mashamba hayo na amewataka wananchi, kuheshimu uwekezaji huo.
Katika hatua nyingine,Mkuu huyo wa mkoa ameipongeza TFS kwa kupanda miti laki saba tangu mvua za masika zilipoanza kunyesha katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Hata hivyo, ameomba kazi hiyo iendelee na iwashirikishe wananchi kwa kutoa ushauri kuhusu miti sahihi inayopaswa kupandwa, badala ya kuacha wananchi wanapanda miti holela na matokeo yake kukauka kutokana na kupandwa sehemu zisizo sahihi.

Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa,Serikali haiwezi kutekeleza kila jambo pekee yake, bali wananchi ni muhimu washirikishwe na washiriki katika shughuli zote za maendeleo kwani hatua hiyo itasaidia kulinda miradi hiyo kwa kuwa wataiona ni yao.

Akizungumza na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Madaba wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Olaph Pili Mkuu huyo wa mkoa alisema, maeneo mengi ya Madaba yana changamoto ya ukataji na uchomaji moto miti,hivyo ni lazima kupanda miti kwa wingi.

Mkuu wa mkoa ameitaka Halmashauri ya Madaba, kutunga na kutumia sheria ndogo zinazomtaka kila mwananchi katika eneo lake kuhakikisha anapanda miti na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaofanya shughuli kwenye vyanzo vya maji na maeneo yasioruhusiwa.
Kuhusu wananchi waliotoa maeneo yao ya kilimo na kuwekwa mipaka (Bikoni) alisema, ni vyema Halmashauri kufanya tathimini ya kina kujua watu wangapi walioathirika ili wapewa maeneo mengine kwa ajili ya kuendelea na shughuli zao.

Amewaonya wananchi walioondolewa katika maeneo ya hifadhi kufanya shughuli zao kutodai fidia yoyote kwani wao ndiyo wenye makosa kwa kuingia na kuvamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya vyanzo vya maji.

Kamanda wa Wakala wa huduma za Misitu Tanzania(TFS)Kanda ya Kusini Manyisye Mpokigwa alisema,TFS ina jukumu la kuhakikisha vyanzo vyote vya maji vinalindwa kwa kushirikiana na wadau wengine wakiwamo mamlaka na wakala za maji(Ruwasa) kwa kupanda miti katika maeneo yote yaliyoathirika na shughuli za kibinadamu.

Naye Meneja wa shamba la miti Wino Glory Kasmir alisema, hadi sasa wamefanikiwa kupanda miti laki saba katika vijiji na maeneo ya ofisi za Serikali kwa ajili ya kurudisha maeneo yaliyoathirika katika hali yake ya asili.
MWISHO.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.