• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

DKT Nchimbi awaongozawananchi kuuaga mwili wa Mzee Songambele

Imewekwa kuanzia tarehe: June 2nd, 2025

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika shughuli ya kuaga mwili wa Hayati Alhaj Mustafa Mohamed Songambele mkoani Ruvuma.

 Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Mzee Songambele Mahenge mjini Songea, Dkt. Nchimbi amesisitiza mchango wa Mzee Songambele katika harakati za kupigania uhuru wa Tanzania, akieleza kuwa alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa Chama cha TANU na alishiriki kikamilifu katika kujenga misingi imara ya taifa jipya baada ya uhuru.

"Tuendelee kujifunza kutoka kwa wazee hawa ambao wamefariki wakiona amani na upendo wa Tanzania ukiendelea, heshima pekee tunayoweza kuwapa ni kuendeleza mshikamano, amani na maendeleo ya nchi yetu, tuendelee kujua sisi ni Taifa moja, tuna wajibu wa kupendana na kujiepusha na vishawishi vyote ambavyo vinaweza vikavuruga amani na kuvunja mtangamano wa kitaifa," alisema Dkt. Nchimbi.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ameguswa sana na msiba huo, akimtaja Mzee Songambele kama kiongozi aliyekuwa na moyo wa kipekee wa kulitumikia taifa kwa hali yoyote hivyo wanaruvuma wana kila sababu ya kujivunia kutokana na mchango wake mkubwa katika kupigania uhuru na kuimarisha maendeleo ya nchi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, ameeleza kuwa kifo cha Mzee Songambele ni pigo kubwa kwa Taifa, akisisitiza kuwa Tanzania imepoteza hazina muhimu ya busara na kumbukumbu hai ya historia yake.

"Hakuwa tu kiongozi bali alikuwa taa na mwelekeo katika giza la ukoloni, aliyesimama kidete kwa ujasiri, hekima, na moyo wa kizalendo katika kuijenga Tanzania mpya alisimama kwa haki, kupitia juhudi zake na  viongozi wenzake wa wakati huo, tunauona leo mwanga wa uhuru, umoja, na amani uliodumu kwa zaidi ya nusu karne," alisema Kanali Ahmed.

Kwa upande wake mtoto wa Hayati Alhaj Songambele, Rajab Songambele, amesema kama familia wataendelea kuyaenzi na kuyafanyia kazi mazuri yaliyofanywa na waliyoachiwa na Mzee wao ili yaendelee kuishi.

Hayati Alhaj Mustafa Mohamed Songambele alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa Chama cha TANU  ambacho kiliasisi harakati za kudai uhuru  akiwa miongoni mwa wanachama wa kwanza 30, na akapewa kadi namba 27, alizaliwa Mei 25, 1925 Bombambili Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma na amefariki akiwa na umri wa miaka 100 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TRILIONI 1.18 za Rais Samia zavunja ukame wa maendeleo Ruvuma,ndani ya miaka minne Ruvuma yachanua

    June 04, 2025
  • RAS RUVUMA alivyowaongoza wananchi kuchangia damu

    June 04, 2025
  • HAYATI SONGAMBELE aacha alama,kitabu chake kuwa rejea kuu ya Taifa

    June 04, 2025
  • MKOA wa Ruvuma kukusanya chupa za damu 14,789

    June 04, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.