• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TIMU ya Majimaji inavyoendelea kuwa kioo cha Mkoa wa Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: February 15th, 2023


MAJIMAJI ni miongoni mwa timu maarufu za soka hapa nchini ambayo ina historia ndefu ukiachia timu za Simba na Yanga ambazo zimedumu kwa muda wote zikicheza ligi kuu bara na kuwa na wapenzi lukuki kila kona ya nchi yetu.

Hakuna ubishi Timu ya Majimaji inafuatia kwa kuwa na washabiki na wapenzi wengi hapa Tanzania.Majimaji katika kipindi chake imepita  katika vipindi vya mafanikio na changamoto.

Licha ya kupata mafanikio makubwa katika mchezo wa soko hapa nchini,Majimaji pia imekumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kushuka daraja mara kadhaa katika vipindi tofauti.

Historia inaonesha kuwa,Klabu ya Majimaji ilianzishwa mwaka 1977 na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wa zamani na Katibu Mkuu Mstaafu CCM hayati Dkt. Rawrence Gama  ambapo   Kikosi  cha kwanza cha Majimaji  kiliweza kuundwa kwa kuichukua timu ya kombaini ya Mkoa wa Ruvuma na kupewa jina la Majimaji.

Kulingana na historia hiyo,Timu ya soka ya Majimaji ilipanda  daraja na kucheza daraja la kwanza kwa wakati huo sasa ligi kuu, mwaka 1982 ambapo walicheza msimu mmoja na kushuka kutokana na wachezaji wake wakati huo hawakuwa na uwezo wa kuhimiri mikikimikiki ya ligi hiyo ambayo ilikuwa na timu nane kwa nchi nzima katika kipindi hicho.

Mwaka 1984 Majimaji ilirejea tena kucheza ligi hiyo kwa kasi baada ya kujipanga na kuwa moja ya timu ambayo ilikuwa na sifa ya kuwalipa fedha nyingi na maslahi bora wachezaji wake ,hali iliyosababisha baadhi ya wachezaji wa timu za Simba na Yanga kutoka Dar es salaam na kutimkia Songea kwa lengo la kujiunga na timu hiyo ya wanalizombe.

Wachezaji ambao walikuwa wakiwika kwa wakati huo kwa timu za Simba, Yanga na Pan African ambao walikuja kujiunga na timu hiyo yenye makao makuu yake mjini Songea, ni  Peter Tino, Zamoyoni Mogela,Malota Soma na Inocenti Haule.

Hata hivyo mchezaji Innocent Haule baadaye aliamua kuachana na Majimaji na kutimkia  nchini Kenya kucheza ligi za huko baada ya uongozi wa Simba kudai wachezaji hao walikuwa wamehama bila kufuata utaratibu wa uhamisho kutoka katika vilabu vyao.

Katika kipindi hicho Timu ya Majimaji ilikuwa tishio kwa vilabu vingine vilivyokuwa vikishiriki ligi hiyo na hata kusababisha kuchukua ubingwa wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa miaka miwili mfululizo mwaka 1985 na 1986 ambapo ligi hiyo ilikuwa ikishirikisha timu sita kati ya hizo timu tatu kutoka Visiwani na tatu kutoka Bara.

Majimaji katika mchezo wake wa kwanza wa mashindano ya klabu bingwa barani Afrika mwaka 1986 ilipangiwa na timu ya Dyanamo ya Zimbabwe, mchezo ambao ulifanyika mjini Harare makao makuu ya nchi ya Zimbabwe, katika mchezo huo Majimaji ilifungwa mabao 5-0.

katika mechi ya marudiano mchezo haukuweza kufanyika kwa sababu Timu ya Majimaji ilijitoa baada ya kupata ajali wakati ikitokea Songea  kuelekea Dar es Salaam na baadhi ya wachezaji wake waliumia vibaya akiwemo Athumani Maulid na ikawa mwisho wake wa kucheza mpira.

Historia inaonesha kuwa,Mwaka wa pili Timu ya Majimaji ilipochukua ubingwa wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ilipangiwa mchezo wake wa kwanza kucheza na timu ya Shirika la Kilimo la nchi ya Madagasca(BTM)  na kushinda bao 2-1.

Katika mchezo wake wa marudiano uliochezwa katika uwanja wa Taifa(Uhuru),jijini Dar es Salaam,Timu ya Majimaji ilishinda tena mabao 2-1 hivyo kusonga mbele, na kutolewa na FC Leopard ya Kenya kwa jumla ya mabao 2-0.

Timu ya Majimaji  ilishuka daraja baada Muasisi wake,Hayati Dkt.Gama kuhama Mkoa wa Ruvuma na kuhamia Mkoa wa Tabora,hali ambayo ilisababisha timu hiyo kuanza kuyumba,baada ya viongozi wa Serikali ya Mkoa  kushindwa kuchangia masuala ya michezo.

 Hayati Dkt.Gama alipenda michezo na alikuwa mstari wa mbele kushughulikia changamoto zilizokuwa zinawakabili wachezaji.Hata hivyo Dkt.Gama akiwa Tabora aliweza kuusaidia Mkoa wa Tabora kuunda timu ya Mirambo iliyokuwa tishio katika ligi kuu Tanzania Bara.

Harakati ya Timu ya Majimaji kurudi tena kucheza ligi kuu Tanzania Bara,zilipata msukumo kutoka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea mjini,Dkt.Emmanuel Nchimbi ambaye alihakikisha kuwa  timu hiyo inarudisha heshima yake ya miaka ya nyuma ambapo alitoa hamasa kubwa kwa  kuwashirikisha  wadau mbalimbali wa soka mkoani Ruvuma na wale wanaoishi nje ya mkoa huo.

Timu ya Majimaji ilijiwekea mikakati iliyosababisha timu hiyo kupanda daraja na kucheza ligi kuu Tanzania Bara katika msimu wa mwaka 2009/2010 baada ya kucheza ligi ya daraja la kwanza Taifa na kufanikiwa kuwa kati ya timu tisa zilizoingia fainali ya kucheza ligi kuu.

Katika fainali hiyo timu tatu zilifanikiwa kuingia ligi kuu kufuatia kushika nafasi za juu katika msimamo wa ligi hiyo,timu hizo ni  Majimaji, Manyema na African Lyon.

Majimaji tangu ilipopanda daraja na kurudi ligi kuu Tanzania bara inajitahidi kucheza.Hata hivyo kiwango cha Majimaji cha enzi zile bado hakijaonekana,hali ambayo inasababisha timu hiyo kushuta tena daraja na kupotea kwenye ukimwengu wa soka.

Hata hivyo  timu hiyo haina budi kuungwa mkono kwa hali na mali ili kuhakikisha kuwa wadau na wafadhili  wanaichangia timu hiyo ili  hatimaye kurudisha heshima ya Majimaji ya enzi zile  katika mchezo wa soka nchini.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.