Na Gustaph Swai-RS Ruvuma
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imetoa elimu kuhusu masuala ya Bima kwa watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Songea.
Mafunzo hayo ya Bima ni sehemu ya jitihada za TIRA katika kutekeleza Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa na Mpango Mkuu wa Taifa wa Kuendeleza Sekta ya Fedha nchini.
Akizungumza wakati anatoa elimu ya Bima kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kamishna wa Bima nchini, Dkt. Baghayo Saqware amesema waamedhamiria kuhakikisha elimu ya bima inawafikia wananchi wengi wa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt.Saqware, ameomba ushirikiano kutoka kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kuhakikisha elimu ya bima inawafikia wananchi wa Ruvuma na kuwajengea uelewa wa kutumia bima kama kinga mahsusi kwa maisha, afya, na mali zao.
"Tunaomba ushirikiano na ofisi yako ili kuhakikisha elimu ya bima inawafikia wananchi wa Mkoa wako kwa lengo la kujenga uelewa wao wa bima ili wabaini manufaa ya kutumia bima kama kinga mahsusi kwa maisha, afya, na mali zao," amesisitiza.
Amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuwa balozi wa TIRA katika utoaji wa elimu ya bima kwa wananchi na kuwahamasisha kutumia bidhaa na huduma za bima hususan bima za afya na kilimo.
Amebainisha kuwa sekta ya bima ina ongezeko la zaidi ya asilimia 10 kwa kila mwaka kwa watoa huduma za bima sambamba na kufanikiwa kuhakikisha ulipaji wa madai ya Bima kwa wakati kwa asilimia 95 na kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma za bima kwa asilimia 20 hadi kufikia mwaka 2023.
Mamlaka ya usimamizi wa Bima (TIRA) imepewa jukumu la kuratibu mambo yote ya kisera yanayohusu bima ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusimamia shughuli zote za Bima Tanzania Bara na Zanzibar.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.