• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TUENDELEE kuchukua tahadhari na magonjwa ya mlipuko-Waziri Mhagama

Imewekwa kuanzia tarehe: September 21st, 2024

Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari juu ya magonjwa ya mlipuko pamoja na magonjwa Yasiyoambukiza.

Waziri Mhagama amesema hayo  alipokuwa akiongea na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya misheni ya Mtakatifu Joseph  Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma  alipofanya ziara ya kikazi  Hospitalini hapo kwa lengo la kujionea hali ya utoaji  wa huduma za Afya.

“Tuendelee kuchukua tahadhari za kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama Mpox, lakini pia kuna magonjwa Yasiyoambukiza kama shinikizo la juu la damu (High Blood Pressure), Kisukari pamoja na magonjwa ya Figo.” Amesema Waziri Mhagama

Aidha, Waziri Mjagama amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa kwenye Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya kwa kuwalipa mishahara watumishi, kununua vifaa, vifaa tiba, kuendelea kujenga wodi za watoto wanaozaliwa na uzito pungufu (NCU).” Amesema Waziri Mhagama

“Kwa dhamana hii aliyonipa Mheshimiwa Rais ya kuitumikia Sekta ya Afya, namuahidi nitaendelea kuitumikia kwa moyo wangu wote, na hii ni heshima yetu kwenye jimbo letu la Peramiho kwa ujumla wake.” Ameahidi Waziri Mhagama

Amesema, kwa mwaka wa fedha 2023/24 Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 3.2 ili kuwaunga mkono Hospitali ya  Rufaa ya Peramiho ambayo imepewa hadhi kuwa Hospitali ya Rufaa kwa kuwa na madaktari bingwa na bobezi.

“Tutaendelea kuzungumza na wadau wengine ili waendelee kuwekeza kwenye Hositali yetu ya Peramiho, tunaishukuru Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation kwa kulipia watumishi Wanne mishahara, huu ni ushirikiano mzuri na wenye tija.” Amesema Waziri Mhagama

Waziri Mhagama amesema, eneo jingine ambalo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amelifanyia kazi kubwa ni kuokoa vifo vya kina mama na watoto pindi wanapojifungua

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe.kapenjama Ndile amesema watoto wanaozaliwa na uzito pungufu wanapata huduma bora na nzuri katika Hospitali ya Rufaa ya Peramiho.

Amesema hospitali hiyo imeonesha namna ambavyo wanaweza kutoa huduma kwa watoto hao wagonjwa ambao wanahitaji uangalizi wa hali ya juu.”


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • BODI ya kwanza ya maji yazinduliwa Tunduru

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.