• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TULILA;kivutio kipya cha uwekezaji na utalii mkoani Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: May 17th, 2021

 

TULILA ndani ya Mto Ruvuma  kata ya Mpepai Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma ambako kumegundulika kuwa vivutio vya kipekee vya utalii na uwekezaji.

  

Hata hivyo maporomoko ya Tulila ndipo kuna mradi wa umeme wa maji toka maporomoko ya mto Ruvuma,unaomilikiwa na watawa wa Benedictine wa Mtakatifu Agnes Chipole Jimbo kuu la songea.

  

Mradi huu unazalisha megawati tano ambazo zilimaliza tatizo la umeme katika mji wa Songea kabla ya Mkoa wa Ruvuma kuingizwa katika grid ya Taifa.

 

Kutoka Songea mjini hadi Tulila ni takribani kilometa 89.Kivutio hiki  bado hakifahamiki na wengi hivyo kinatakiwa kutangazwa ili kifahamike ndani na nje ya nchi.

 

Tulila ni eneo lenye mandhari nzuri ya kuvutia unaweza kufanya utalii wa kupiga picha, kuogelea, kuendesha mtumbwi pia kuna fukwe nzuri kutoka katika mto Ruvuma.

  

Uchunguzi umebaini kuwa bwawa la kuzalishaji umeme lenyewe pekee ni kivutio tosha cha utalii wa majini na katika eneo hili kuna aina adimu za ndege ambao ni kivutio cha utalii wa kuona ndege.

  

Utalii ambao unaweza kushamiri hivi sasa katika Mkoa wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla ni utalii wa ndani ambapo katika eneo la Tulila watawa wanamiliki eneo lenye ukubwa wa hekari 1000.

  

Watawa katika eneo la bwawa wamewekeza kwenye ufugaji wa samaki wa aina mbalimbali na kupanda miti aina ya mitiki yenye thamani kubwa kwa sababu hekari moja ya mitiki inaweza kumuingizia mkulima hadi shilingi milioni 400.

  

Afisa Maliasili na Utalii Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe anasema uchunguzi umebaini kuwa samaki hao wanavutia makundi ya ndege wakiwemo  tai ambao wanakula samaki.

 

 Watawa hao wanafuga mbuni ,bata mzinga na aina nyingine za ndege ambao ni kivutio cha utalii ambapo Tulila itakuwa maalum kwa ajili ya utalii wa kuona ndege wa aina mbalimbali.

  

Maporomoko ya Tulila yapo kilometa sita toka Pori la Akiba la Liparamba lenye wanyama wa aina mbalimbali hivyo watalii watakaotembelea Liparamba wanaweza kufika kwenye maporomoko ya Tulila ambako wanaweza kupata malazi na chakula kwenye  hoteli za kisasa za kitalii zinazomilikiwa na watawa hao.

  

Inaelezwa tembo wa Liparamba pia wanafika kwenye maporomoko ya Tulila  na kwamba majira ya asubuhi na jioni makundi makubwa ya ndege na viboko wanafika katika eneo hilo kunywa maji na kula chakula.

  

Mto Ruvuma ambao Chanzo chake ni milima ya Matogoro iliyopo nje kidogo ya mji wa Songea,ni miongoni mwa mito maarufu barani Afrika unamwaga maji yake Bahari ya Hindi .

  

Imeandikwa na Albano Midelo

 

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

 

Mei 17,2021

 


   

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.