Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma inaendelea kupiga hatua kubwa katika utekelezaji wa afua za lishe, kama ilivyobainishwa katika kikao cha kawaida cha kamati ya lishe wilaya kwa robo ya pili (Oktoba-Disemba)
Kikao hicho kilionesha mafanikio makubwa katika utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha lishe na afya ya wananchi.
Miongoni mwa mikakati inayotekelezwa ni Mpango Mkakati wa Lishe na Afya Shuleni, ambapo shule zote za msingi na sekondari zinazomilikiwa na serikali kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni.
Mikakati mingine ni Kwa shule za kutwa, wazazi wanahamasishwa kuchangia kupitia kamati zao ili kufanikisha mpango huu.
Pia, elimu inaendelea kutolewa kwa shule za msingi na sekondari kuhusu lishe bora. Wanufaika wa Mradi wa TASAF wenye watoto chini ya miaka mitano wanahamasishwa kuwapeleka watoto kliniki kwa ajili ya ufuatiliaji wa afya zao.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Ndg. Bosco Mwingira, alisisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ulaji unaofaa na mtindo bora wa maisha ili kuzuia magonjwa sugu yasiyoambukiza.
Mwingira amesema halmashauri inahamasisha kilimo cha mbogamboga na matunda ili kuongeza upatikanaji wa vyakula vyenye virutubisho.
Ameshauri kufanyika ufugaji wa samaki bora, ambapo visima viwili vya samaki vimechimbwa katika kijiji cha Kidugalo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.