Katika hatua ya kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, kupitia Mkuu wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe, Dr. Wilfred Rwechungula,amefanya kikao maalum na wasimamizi wa vituo vya afya na zahanati. Kikao hiki kimelenga kuwakumbusha wajibu wao katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na za uhakika.
Miongoni mwa mada zilizoshirikishwa katika kikao hicho ni pamoja na umuhimu wa kujaza taarifa za wagonjwa kwa usahihi ili kuepuka makosa yoyote.
Wasimamizi wamepewa mafunzo ya ziada kuhusu utoaji wa huduma za UKIMWI, kufuatilia viashiria vya maradhi, na kuhakikisha kuwa watu wanaoishi na UKIMWI wanapata matibabu na huduma bora.
Kikao hicho kimesisitiza kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto .
Akizungumza katika kikao hicho, Dr. Rwechungula amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wasimamizi na watendaji wengine wa afya ili kuhakikisha kila mgonjwa anapata huduma anayostahili kwa wakati.
Kwa upande wao, wasimamizi wa vituo vya afya wameahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa katika kikao hicho ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata afya bora.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.