WAKULIMA wa zao la ufuta wilayani Tunduru,wamefanikiwa kuingiza Sh.bilioni 17,131,112,080.6 baada ya kuuza tani 4,641 sawa na kilo milioni 4,641,473.7 za ufuta ghafi kupitia minada 6 iliyofanyika kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani wilayani humo.
Hayo yamesemwa j na Afisa Masoko wa Chama Kikuu cha Ushirika(TAMCU Ltd) wilaya ya Tunduru Marcelino Mrope kwenye mnada wa sita wa zao hilo uliofanyika katika Chama cha msingi cha Ushirika Mlimi(Amcos)kijiji cha Misechela.
Alisema,katika mnada wa sita uliofanyika kijiji cha Misechela wakulima wameuza zaidi ya tani 240.8 za ufuta sawa na kilo 240,818.5 zenye thamani ya Sh.milioni 836,362,650.5.
Aidha alisema,katika mnada wa tano uliofanyika kijiji cha Namwinyu jumla ya tani 770 za ufuta wenye thamani ya Sh.bilioni 2,678,000.00 uliingizwa sokoni ambapo bei ya wastani ilikuwa Sh.3,475 kwa kilo moja.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika TAMCU Ltd Mussa Manjaule,amewapongeza wakulima kwa kubuni mazao mbadala ya biashara ikiwemo zao la ufuta ambalo limewaingizia fedha nyingi katika kipindi kifupi.
Alisema,hatua hiyo ni mafanikio makubwa na kuwasisitiza kulima kilimo cha kisasa kwa kufuata maelekezo ya wataalam na kuongeza ukubwa wa mashamba yao ili kujikomboa na umaskini kupitia shughuli zao za kilimo.
Manjaule amewataka wakulima wa ufuta na mazao mengine,kutumia fedha wanazopata kufanya mambo ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa nyumba za kisasa na kusomesha watoto wao na kuepuka kutumia fedha kwenye mambo ya anasa ambayo ni adui mkubwa wa maendeleo.
Naye Afisa Ushirika wa wilaya ya Tunduru Geroge Bisan alisema,zao la ufuta limeendelea kufanya vizuri kutokana na uzalishaji wake kuongezeka mwaka hadi mwaka hali iliyopelekea hata bei kuwa nzuri ikilinganisha na miaka ya nyuma.
Amewasihi wakulima kutumia ardhi yao vizuri kwa kuongeza uzalishaji wa mazao mashambani na kuepuka kuuza ardhi ovyo kwa wageni walioanza kuingia kwa wingi katika wilaya hiyo kutafuta ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo na biashara.
Badala yake waitumie wao wenyewe kuzalisha kwa wingi mazao mbalimbali ya chakula na biashara kama njia pekee ya kuondokana na umaskini kwenye familia zao.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima wenzake Kitanda Rashid,ameipongeza serikali kusimamia uuzaji wa zao la ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani kwani umekuwa mkombozi mkubwa kwa wakulima.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.