• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TUNDURU waomba kufanyiwa uchunguzi vimelea vya kifua kikuu

Imewekwa kuanzia tarehe: March 30th, 2023

WANANCHI wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,wameiomba serikali kupitia Wizara ya Afya kuwa na utaratibu wa kutembelea mara kwa mara maeneo ya vijijini kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzina upimaji wa vimelea vya ugonjwa kifua kikuu na kuwaanzishia dawa watakaobainika kuwa na  maambukizi ya ugonjwa huo.

Wametoa ombi hilo wakati wa kampeni ya uchunguzi wa ugonjwa huo iliyofanywa na wataalam kutoka Hospitali ya wilaya Tunduru kupitia kitengo cha kifua kikuu na ukoma kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo shirika lisilo la Kiserikali la MDH-Amref Health Africa.

Kampeni imefanyika katika kijiji cha Chingulungulu kata ya Muhuwesi na kuhudhuriwa na wananchi kutoka vijiji vya kata jirani ya Majimaji,Sisi kwa Sisi iliyoambatana na maadhimisho ya siku ya kifua kikuu Duniani ambayo kimkoa imefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Ngatuni wilayani Tunduru.

Hadija Jaribuni alisema,utaratibu wa kupeleka huduma za uchunguzi wa afya kwa wananchi waishio maeneo ya pembezoni ni nzuri sana kwani utasaidia kuokoa maisha ya watu wengi hasa wanaoishi maeneo  hayo ambayo ni nadra sana kufikiwa na huduma hizo kwa wakati.

“naishukuru sana serikali  kupitia Hospitali ya wilaya Tunduru kitengo cha kifua kikuu na ukoma kutuletea huduma ya uchunguzi,tunaomba wataalam wafike mara  kwa mara”alisema Jaribuni.

Ameishukuru serikali kupeleka huduma hiyo kwa wananchi ambao hawana uwezo wa kwenda Hospitali na vituo vya kutolea huduma  kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya zao na kupata matibabu.

Shamila Said alisema,kufikishwa kwa huduma ya uchunguzi kwenye maeneo ya vijijini itasaidia sana kuokoa maisha ya watu wengi hasa wazee ambao hawawezi kufika kwenye vituo vya kutolea huduma kutokana na sababu mbalimbali  ikiwemo kukosa nauli ya kutoka kijijini hadi Hospitali ya wilaya Tunduru mjini.

Alisema,huduma  ya uchunguzi wa vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu ni nzuri kwani inatoa majibu ya shida za wananchi wenye maradhi ambao wana tabia ya kumeza dawa bila kupata ushauri wa Madaktari.

Diwani wa kata ya Muhuwesi Iman Ngonyani alisema,wananchi wa kijiji cha Chingulungulu wameanza ujenzi wa zahanati ambayo mara itakapokamilika itasaidia kutoa huduma mbalimbali za matibabu ikiwemo huduma ya uchunguzi wa ugonjwa wa kifua kikuu.

Ngonyani,amewapongeza watoa huduma kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwataka kuendelea kuwasaidia wananchi ambao bado wanakabiliwa na changamoto nyingi za kimaisha  na maradhi ya mara kwa mara.

Kwa upande wake Mratibu wa ugonjwa wa kifua kikuu na ukoma wa wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole alisema,katika kampeni ya mwaka huu  nguvu kubwa imeelekezwa kutoa elimu ya kifua kikuu kwa wanafunzi kutokana na kundi hilo kuwa katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo.

Alisema,wanafunzi wakipata elimu kuhusu ugonjwa huo itakuwa rahisi kuchukua tahadhari na hata kupeleka elimu hiyo kwa wazazi wao na jamii kwa ujumla.

Dkt Mkasange aliyataja makundi mengine yaliyoko kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa TB ni wafugaji,wasafiri,wafungwa,watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na wale wanaishi kwenye makazi duni.

Mkasange,ameitaka jamii kuwa na utaratibu wa kwenda katika vituo vya kutolea huduma na Hospitali kwa ajili ya uchunguzi ili kufahamu hali za afya zao badala ya kuwa na mazoea ya kumeza dawa bila kupata ushauri wa wataalam

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.