Kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu zoezi la uandikishaji daftari la wakazi lafikia asilimia 45 ikiwa ni siku nne tangu kuanza kwa zoezi hilo nchini.
Hayo yamebainishwa l na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
“Nawapongeza watanzania waliojitokeza kujiandikisha tangu kuanza kwa zoezi hili Octoba 11 kwani hatua hii ni muitikio mzuri wa watanzania kutambua haki yao ya kikatiba ya kujiandikisha kwaajili ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa”, amesema Mh.Mchengerwa
Aidha, ametumia fursa hiyo kuwahimiza watanzania wote wenye sifa za kupiga kura kuendelea kujitokeza kujiandikisha kwani zoezi hilo litakamilika Octoba 20, 2024.
Ameeleza kuwa katika zoezi hilo la uandikishaji baadhi ya Mikoa inaendelea kufanya vizuri ikiwemo Tanga,Ruvuma,Njombe,Songwe na Iringa.
“Kuna mikoa ipo chini ya wastani unaokusudiwa ikiwemo Katavi, Kilimanjaro,Geita,Kigoma na Manyara, pia ipo mikoa yenye watu wengi lakini uandikishaji bado uko chini ya asilimia 40 ambayo ni Dar es salaam iko kwenye asilimia 35.3,Mwanza ina asilimia 34.2,Morogoro iko kwenye asilimia 37.9,Dodoma asilimia 38.5,Tabora asilimia 27.7 pamoja na Kagera asilimia 34.8”, amesema Mh.Mchengerwa
Mwisho amewasihi Wakuu wa Mikoa na viongozi wa Halmshauri kuendelea kuwahimiza watanzania kujitokeza kwaajili ya kujiandikisha kwenye daftari la makazi litakalotumika katika uchaguzi wa Serikali za mitaa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.