Ubalozi wa Finland Nchini Tanzania umeridhishwa na Mradi wa Panda Miti kibiashara unaotekelezwa katika Wilayani Nyasa.
Hayo Yamesemwa leo na Mshauri wa Mradi, wa wa uendelezaji wa mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu (Forvarc) kutoka Bw Juhan Harkonen, Aliyetembelea na kukagua Mradi wa Panda Miti kibiashara unaotekelezwa na wananchi wa Kata ya Liuli Wilayani Nyasa.
Bw Juhan amefafanua kuwa amekagua na kuridhishwa na maendeleo ya Mradi wa Panda miti kibiashara, baada ya kuona maendeleo yake ni mazuri na wananchi wamehamasika na kuitikia wito wa kupanda miti katika Safu ya Milima ya Livingstone Wilayani Nyasa.
Ametoa wito kwa wananchi kuendelea na Mradi huo kwa kuwa utawapa maendeleo makubwa ya kipato cha kaya na Taifa kwa ujumla.
Awali Akiwakaribisha wageni hao kutoka Ubalozi wa Finland ambao ni wafadhili wa Mradi , kupitia Program ya Forvac, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh Isabela Chilumba amewapongeza wananchi wa Kata zote Wilayani Nyasa zinazotekeleza Mradi Licha ya kuwa kupata vikwazo mbalimbali wameendelea kutekeleza Mradi huu kwa lengo la kuwa na zao la Kibishara, ili kuondokana na Umaskini na kujiongezea kipato, cha kaya na mapato ya Halmashauri.
Ameongeza kuwa Wilaya ya Nyasa inawashukuru wafadhili hao kwa kufadhili mradi wa pandamiti Kibiashara ambao utaleta tija kwa wananchi wa Nyasa na Taifa kwa Ujumla.
Ametoa Wito kwa wafadhili hao kufadhili miradi mingine kama ya Maji na Utalii kwa kuwa Wilaya hii ina uhitaji wa Ufadhili katika Sekta hizo.
Naye Mwenyekiti wa Kikundi cha Upandaji miti kibishara katika kata ya Liuli Bw Samweli Mawanja amewapongeza wafadhili hao kwa kufadhili mradi huo na amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Nyasa na Mkururugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa kwa Kusimamia vema Mradi huu.
Ujumbe huu kutoka Ubalozi wa Finland Nchini Tanzania umeambatana na Mshauri wa Mali Asili kutoka Ubalozi wa Finland Nchin Tanzania, Hein Vihemak na Mratibu wa kitaifa wa Forvac kutoka Wizara ya MaliAsili na Utalii.
Imeandikwa na Netho Kredo
Afisa Habari wilaya ya Nyasa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.