• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

UFUTA wawaingizia wakulima Ruvuma bilioni 16.8

Imewekwa kuanzia tarehe: June 10th, 2020

WAKULIMA wa zao la ufuta katika Wilaya za Namtumbo,Songea na Tunduru mkoani Ruvuma wameanza kunufaika na zao hilo baada ya kupokea shilingi bilioni 16.8 tangu kuanza kuuza zao hilo kwa mfumo wa stakabadhi ghalani Apirili 30 mwaka huu.

Hayo yamesemwa na  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme  wakati anafungua kikao maalum cha Baraza la madiwani la Halmashauri ya Namtumbo cha kujadili Hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

“Mpaka sasa katika minada ya Songea,Namtumbo na Tunduru zimeuzwa kilo milioni 8.2 za zao la ufuta zilizosababisha wakulima kupata sh.bilioni 16.8 ambazo zitaendelea  kuongezeka kupitia minada inayokuja’’,alisisitiza Mndeme.

Mndeme amesema tangu kufunguliwa kwa mnada, vyama  vya ushirika AMCOS kupitia zao la ufuta vimekwishapata  zaidi ya sh.milioni 500 na ushuru uliopatikana kwenye vyama vikuu  vya ushirika SUNAMCO na TAMCO ni shilingi  milioni 2.48.

Amesisitiza kuwa  Mkoa wa Ruvuma umeendelea kuonesha mafanikio makubwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani na kwamba mfumo huo utaendelea kutumika kwenye mazao ya soya na Mbaazi ili  kulinda haki ya wakulima.

 Mndeme amesema  Mkoa wa Ruvuma msimu huu unatarajia kuendelea kuwa gwiji katika mazao ya chakula ambapo  mahitaji ya chakula katika Mkoa wa Ruvuma ni tani laki 3.38 hadi sasa Mkoa  una ziada ya chakula zaidi ya tani laki tisa.

Amesisitiza kuwa Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa inayofanya vizuri katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara nchini  na kwamba  hadi kufikia Mei 15 mwaka huu  zilikuwa zimevuna tani milioni  1.3.

Wakati huo huo Mndeme  amewapongeza Halmashauri ya Namtumbo kwa kupata hati safi ya ripoti ya CAG kwa miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2015/2016 hadi 2018/2019.

Mndeme amewapongeza Madiwani na watalaam kwa kuweza kuchangia asilimia 99.77 katika mfuko wa wanawake,wazee,vijana na watu wenye ulemavu na   kukusanya mapato ya ndani Zaidi ya Sh. bilioni 1.94 katika mwaka wa fedha wa  2018/2019.

Imeandaliwa   Albano Midelo

Afisa Habari wa Mkoa wa Ruvuma

Juni 10,2020

Namtumbo

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.