• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

UGONJWA wa usubi bado tishio mkoani Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: August 7th, 2023

UGONJWA wa usubi umetajwa kuwa bado ni tishio kwa wananchi mkoani Ruvuma.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele mkoani Ruvuma, Dr.Charles Hinju  kwenye mafunzo ya kudhibiti na kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika jamii kwa wajumbe wa RHMT.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mipango Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,mjini Songea,Dr.Hinju ameitaja Wilaya ya Nyasa kuwa inaoongoza kwa maambukizi ya ugonjwa wa usubi kwa asilimia 18.

“Katika zoezi la utafiti la kuchukua damu kwa Watoto wadogo kuanzia miaka mitano Kwenda tisa,lilionesha kuwa katika Mkoa wa Ruvuma asilimia 4.2 walikuwa na ugonjwa wa usubi,wilaya ya Nyasa pekee ilionekana ina maambukizi makubwa ya asilimia 18.33’’,alisisitiza Dr.Hinju.

Kutokana na tishio la maambukizi ya ugonjwa wa usubi,Mkoa mwezi huu Agosti umedhamiria kutoa dawa za kinga tiba ya  magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele katika jamii katika wilaya zote.

Hata hivyo amesema kwa mwaka huu kipaumbele kitakuwa zaidi kwa ugonjwa wa usubi ambapo viongozi ngazi ya wilaya na Mkoa wataandaliwa Pamoja na kuhamasisha jamii ili kufahamu zoezi zima la ugawaji dawa kinga kwa jamii litakavyofanyika.

Amesisitiza kuwa dawa kinga hizo zitatolewa kwa wananchi wote ambao wanapaswa kunywa dawa wenye umri wa kuanza miaka mitano na kwamba dawa hizo hazitatolewa kwa akinamama wajawazito na wagonjwa  wenye magonjwa waliolazwa ambao hawahitajiki kunywa dawa hizo.

Amesema asilimia 80 ya jamii inahitajika kupata dawa kinga hizo ili kukabiliana na maambukizi ya  ugonjwa wa usubi ambao amesema unaleta athari kwenye Ngozi,macho na kuhusisha ugonjwa wa kifafa.

Ametoa rai kwa jamii kuhakikisha kuwa wanakunywa dawa kinga hizo ili kukabiliana na usubi kwa sababu ugonjwa wa usubi katika Mkoa wa Ruvuma ni changamoto kubwa.

Kwa mujibu wa Dr.Hinju,utafiti uliofanyika mwaka 1997 ulionesha kuwa asilimia 40 hadi 71 waligundulika kuwa maambukizi ya ugonjwa wa usubi mkoani Ruvuma.

Utafiti mwingine uliofanyika mwaka 2011 mkoani Ruvuma kuhusiana na ugonjwa wa usubi ,ilibainika kuwa asilimia 4 walikuwa na usubi na kwamba hali ilikuwa mbaya zaidi katika wilaya ya Nyasa iliobainika kuwa na maambukizi makubwa.

Dalili za ugonjwa wa usubi ni  Mgonjwa kupata viupele upele kwenye ngozi yake ya mwili,Mgonjwa kupatwa na shida ya upofu wa macho,Mgonjwa kupatwa na miwasho ya mara kwa mara kwenye ngozi yake ya mwili,Joto la mwili kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa,Mgonjwa kukosa hamu ya kua chakula na Ngozi ya mwili kuchuchuka

Wizara ya Afya imedhamiria kuendeleza juhudi za kumezesha kinga tiba pamoja na utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu ugonjwa wa usubi ili kufikia lengo la mwaka 2030 ugonjwa huo uweze kutokomezwa.
Ugonjwa wa usubi unaathiri ngozi ya binadamu, kupatwa na homa kali, kutokwa na vipele mwilini, kuhisi uwasho mkali pia unaweza kusababisha upofu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya,ugonjwa wa usubi umeenea katika Halmashauri 29 ambapo takribani asilimia 7.02 ya watu wapo katika hatari ya maambukizi ya ugonjwa huu nchini. Magonjwa mengine ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele na yanadhibitiwa kwa ugawaji dawa ni matende, trakoma, kichocho,minyoo ya tumbo na usubi.

Mikoa mingine nchini inayokabiliwa na ugonjwa wa usubi ni Tukuyu mkoani Mbeya ,Mahenge mkoani Morogoro na Mkoa wa Tanga.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.