Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema uhamasishaji mkubwa umefanyika kupitia “Royal Tour” na mpango Mkakati umeandaliwa na maeneo ya vivutio yamefanyiwa maboresho hivyo kuvutia watalii.
Kanali Thomas ameyataja miongoni mwa maeneo yaliyoboreshwa kuwa ni kuongeza wanyamapori katika bustani ya Ruhila Songea na kupeleka wanyamapori katika kisiwa cha Lundo Mbambabay wilayani Nyasa na kwamba limepelekwa boti kwa ajili ya kuwapeleka watalii katika kisiwa cha Lundo na Mbambabay.
Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa nchini ambayo imebarikiwa kuwa na vivutio vya utalii vya aina zote.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.