• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

UJENZI barabara ya lami Likufusi-Msumbiji waiva,Makamu wa Rais aagiza mkataba usainiwe mwezi huu

Imewekwa kuanzia tarehe: July 22nd, 2023

SERIKALI inatarajia kuanza mradi wa ujenzi wa barabara ya lami nzito ya mpakani mwa Tanzania na Msumbiji yenye urefu wa kilometa 124 kutoka Likuyufusi hadi Mkenda  wilayani Songea mkoani Ruvuma.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya wakati anatoa maelezo ya kuanza kwa mradi huo kwa Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango ambaye yupo mkoani Ruvuma katika ziara ya kikazi ya siku tano.

Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Peramiho,Mhandisi Kasekenya amesema Ruvuma ndiyo Mkoa pekee nchini uliopo mpakani ambao barabara zake hazijaunganishwa kwa  lami na nchi jirani ambapo amesema barabara hiyo iliyopo kwenye Ilani ya CCM,sasa inatekelezwa na serikali ya Sita katika mwaka huu wa fedha.

“Mheshimiwa Makamu wa Rais na wananchi wa Jimbo la Peramiho napenda kuwahakikishia kuwa Rais Samia Suluhu Hassan mwaka huu wa fedha, ameshatoa kibali cha kuanza kujenga barabara ya Likuyufusi-Mkenda na Mkandarasi ameshapatikana kuanza kujenga kipande cha kwanza chenye urefu wa kilometa 60 toka Likuyufusi hadi Muhukuru’’,alisema.

Naibu Waziri huyo wa Ujenzi na Uchukuzi amesema kinachosubiriwa hivi sasa ni kusainiwa mkataba wa kuanza ujenzi wa barabara hiyo na kwamba  taratibu zote za kuanza ujenzi wa barabara hiyo zimekamilika.

Amesema katika utekelezaji wa mradi huo serikali imetoa shilingi bilioni 60 kuanza kujenga barabara hiyo,pia serikali  imetoa shilingi bilioni 22 kujenga daraja imara la Mkenda kwenye mto Ruvuma ili kuwezesha kupita magari makubwa na madogo.

Amesema serikali pia imetoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 18 kujenga daraja katika eneo la Mitomoni katika Mto Ruvuma linalounganisha wilaya za Songea na Nyasa na kwamba kinachosubiriwa hivi sasa ni kusainiwa mkataba wa kuanza ujenzi wa daraja hilo.

Akizungumza na wananchi hao wa jimbo la Peramiho Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango amemuagiza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kusaini mkataba huo ndani ya mwezi Julai mwaka huu kwa kuwa kila kitu kimekamilika na Mkandarasi amepatikana hivyo mradi uanze kutekelezwa mara moja.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo mkoani Ruvuma katika ziara kikazi ambapo hadi sasa amekagua miradi na kusalimiana na wananchi katika wilaya za Songea na Namtumbo.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.