Serikali ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kuanza ujenzi wa daraja la Mitomoni katika Mto Ruvuma linalounganisha Wilaya ya Songea na Nyasa mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Innocent Bashungwa akizungumza bungeni Dodoma amesema Wizara hiyo ipo mbioni kuanza kujenga daraja la kisasa na la kudumu katika eneo hilo linalounganisha vijiji vya Mitomoni wilayani Songea na Kijiji cha Mipotopoto wilayani Nyasa.
“Maandalizi ya nyaraka kwa ajili ya kutangaza zabuni kwa mara ya pili kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mitomoni yamefikia hatua za mwisho na zabuni zitatangazwa mwezi Juni mwaka huu’’,alisema Bashungwa.
Waziri Bashungwa amesisitiza kuwa serikali ya Rais Samia ipo na wananchi wa Wilaya ya Nyasa na Songea na kwamba kufikia Juni mwaka huu ujenzi wa daraja hilo unatarajia kuanza.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.