• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

UJENZI hospitali ya Mbinga wafikia asilimia 98,huduma zaanza kutolewa

Imewekwa kuanzia tarehe: February 17th, 2023

MRADI wa ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya wilaya Mbinga mkoani Ruvuma unaotekelezwa kwa gharama ya Sh.bilioni 1.5 umefikia asilimia 98 ya utekelezaji wake.

Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo George Mhina amesema,hadi sasa majengo matano kati ya saba ambayo ni maabara,jengo la wangonjwa wa nje(OPD),kichomea taka,jengo la mionzi,jengo la bohari ya dawa na la kufuria yamekamilika.

“katika awamu ya tatu ambayo ni ya mwisho tutajenga jengo la wodi ya wazazi ambalo ndani yake kutakuwa na huduma ya upasuaji na kulaza akina mama wanaotoka kujifungua na jengo la utawala,tuko  hatua ya mwisho ya kumpata mkandarasi atakayejenga jengo hilo”amesema Mhina.

Amesema,Hospitali hiyo itakapo kamilika itahudumia zaidi ya watu 255,000 kutoka vijiji vya Halmashauri ya Mbinga na wananchi wa wilaya jirani ya Songea na Nyasa.

Hali kadhalika amesema,kwa sasa wameanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje,hata hivyo matarajio yao katika kipindi cha miezi mitatu ijayo,waanze kutoa huduma ya upasuaji kwa akina mama wajawazito hasa wale watakaoshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.

Pia amesema,mwishoni mwa mwezi huu,wataanza kutoa huduma za mionzi( X-ray) na Ultrasound kwa kuwa jengo lake limekamilika na wanachosubiri kupata vifaa kutoka bohari ya dawa nchini(MSD)yenye dhamana ya kusambaza dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya kutoa huduma za matibabu vya serikali.

Amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutoa fedha ambazo zinatumika katika utekelezaji wa mradi huo na miradi mingine ya maendeleo kwa Halmashauri ya Mbinga.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Amad Mwalukunga amesema,kuanza kwa huduma katika Hospitali  hiyo kumewasaidia wananchi wa Halmashauri ya wilaya Mbinga kumaliza kero ya kwenda hadi  Hospitali ya St Joseph Peramiho  umbali wa kilomita 80 na Hospitali ya wilaya Mbinga iliyopo umbali wa km 20 kufuata matibabu.

Dkt Mwalukunga ametaja magonjwa yanayowasumbua wananchi wa ukanda wa Kigonsera ni malaria na hali hiyo inatokana na asilimia ni wakulima ambao wakati huu wa masika wengi wao wanaishi mashambani ambako wanakutana na changamoto ya kuumwa na mbu wanao sababisha ugonjwa huo.

Ameiomba Serikali kuitupia jicho Hospitali na kutoa fedha ambazo zitawezesha kukamilisha kabisa ujenzi wake ili wananchi waweze kupata huduma zote muhimu, badala ya kwenda maeneo mengine.

Mmoja wa wananchi aliyekutwa akipata matibabu Nassibu Mapunda,ameishukuru Halmashauri ya wilaya Mbinga kujenga Hospitali hiyo kwani licha ya kutokamilika,wameanza kupata huduma karibu na kupata muda kufanya  kazi nyingine za kiuchumi.

Mapunda amesema,hapo awali walikuwa kwenye mateso makubwa ya kwenda Halmashauri nyingine kwa ajili ya kufuata matibabu, lakini sasa wanafurahi kuona baadhi ya huduma hizo  zinapatikana karibu na makazi yao.

Hata hivyo,Mapunda ameiomba serikali kuwajengea barabara ya kutoka  barabara kuu ya Songea-Mbinga hadi Hospitali kwa kiwango cha lami au changarawe ili kurahisisha usafiri wa kufika Hospitali.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.