Mfuko wa Global Fund umetoa zaidi ya shilingi milioni 545 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya kata ya Mletele katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mjini mkoani Ruvuma.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispa ya Songea Dkt Frederick Sagamiko kwa kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma .
Dkt. Sagamiko amebainisha kuwa ujenzi huo unahusisha kujenga Jengo la upasuaji,wodi ya wazazi, Maabara, nyumba ya Mganga, chumba cha kuhifadhi maiti pamoja na Vyoo vya nje.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa mradi huu unatekelezwa kwa kutumia nguvu za wananchi ambao wamechangia zaidi shilingi milioni saba ambapo mpaka sasa fedha zote zimetumika na mradi umekamilika kwa asilimia 100.
“Wananchi wa Kata ya Mletele na Kata za jirani wameanza kunufaika na mradi huu kwa kuwasogezea huduma ya afya karibu”,amesema Sagamiko.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Komred Oddo Mwisho ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayongozwa na Rais Dkt samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusimamia sekta ya afya ambayo inawasaidia wananchi kupata huduma kwa haraka na ubora.
Imeandikwa na Farida Baruti
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.