MKuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas Mei 16,2023 ameendelea na ukaguzi wa miradi ya barabara za TARURA katika Wilaya ya Songea kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya lami nyepesi kutoka Heroes Lizabon hadi Mjimwema Halmashauri ya Manispaa ya Songea yenye urefu wa kilometa 1.3 iliyotengewa zaidi ya shilingi milioni 439.
Mkuu wa Mkoa ameendelea kusisitiza usafi katika maeneo ya barabara hasa kwenye mifereji ya maji huku akitoa rai kwa wananchi wanaoishi kando kando mwa barabara kufanya usafi wa mazingira Mara kwa mara.
Kanali Laban Thomas ameipongeza serikali ya Awamu ya Sita kwa kufanya Uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu ya barabara kupitia TARURA mkoani Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.