Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji zilizosambazwa kupitia mitandao ya kijamii hivi karibuni kuwa mgonjwa alilitozwa Shilingi Laki Mbili (200,000/-) ikiwa ni gharama ya usafiri wa ambulance kupelekwa Hospitali ya Mt. Joseph Peramiho.
Kulingana na Sera ya Afya ya Serikali, hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea haitozi malipo kwa wagonjwa wanaopelekwa Hospitali ya Mt. Joseph Peramiho kwa rufaa, ingawa kwa wagonjwa wanoomba wenyewe kuhamia hospitali ya Mt. Joseph Peramiho familia hulazimika kuchangia Shilingi 21,000 ikiwa ni gharama ya mafuta ya ambulance.
Kuhusu wagonjwa wanaopelekwa Muhimbili au hospitali za kanda kwa rufaa, hulazimika kuchangia mafuta ya ambulance pekee kulingana na umbali. Aidha hospitali huwajibika kulipa posho kwa dereva na muuguzi wanaomsindikiza mgonjwa.
Hospitali inapenda kuufahamisha umma kuwa hakuna mgonjwa aliyepokelewa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea na kupewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Mt. Joseph Peramiho kwa ambulance.
Sera ya Afya ya Serikali (2007) inasisitiza utoaji wa huduma za afya kwa usawa, bila ubaguzi, na kwa misingi ya haki. Huduma za matibabu maalum zinazohitaji rufaa zinapaswa kutolewa kwa utaratibu unaohusisha michango kidogo ya mafuta kwa familia, lakini malipo ya ziada ni kinyume na sera hiyo.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea inatoa huduma kwa kufuata utaratibu wa Sera ya Afya ya Serikali. Tunatoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu na kuepuka kueneza taarifa zisizo sahihi kuhusu huduma za afya za umma.
Imetolewa na:
Dkt. Magafu Majura
MGANGA MFAWIDHI
HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SONGEA
Kwa maelezo zaidi piga namba yetu ya huduma kwa wateja simu 0737683544
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.