Katika kijiji cha Litembo wilayani Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, kuna kivutio cha kipekee kisicho na mfano – masalio ya unyayo wa mguu wa kulia wa binadamu ulioachwa juu ya jiwe mnamo mwaka 1902, muda mfupi baada ya mauaji ya kikatili ya zaidi ya mashujaa 800 wa kabila la Wamatengo waliopigwa risasi na wajerumani kwa bunduki 19, wakipinga ukoloni kwa ujasiri wa hali ya juu.
Mashuhuda wanasema mtu huyo alikanyaga kwa nguvu baada ya kuona damu nyingi ya mashujaa ikitiririka kama mto kwenye kijito cha Mapipi.
Kwa zaidi ya miaka 100, maji ya mto huo hayakutumika na jamii, kutokana na hofu na heshima kwa damu ya mashujaa walioimwaga kwa ajili ya uhuru wetu.
Ili kuihifadhi historia hii na kumuenzi kila mmoja wa mashujaa hao, wananchi wa Litembo wanaiomba Serikali kujenga Makumbusho ya Kisasa kwenye jengo la kihistoria la chifu lililojengwa na wakoloni mwaka 1933 katika kijiji cha Litembo – jengo ambalo limekuwa kitovu cha kumbukumbu ya ukombozi wa Wamatengo na urithi wa kishujaa wa Taifa.
Tukumbuke, tusimame, tuenzi historia yetu – kwa heshima ya mashujaa wa Litembo, kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.