Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma Mheshimiwa Ngollo Malenya, ametembelea Kata ya Litola baada ya upepo mkali kuharibu makazi ya wananchi, ikiwemo nyumba 6 za walimu na vyoo 10.
Ziara hiyo imelenga kutathmini hali halisi na kuwapa pole waathirika wa tukio hilo.
“ wananchi hakikisheni mnazingatia ubora wa ujenzi wa nyumba zao ili kupunguza madhara yatokanayo na majanga ya asili”,alisema Malenya
Ameeleza kuwa nyumba imara zinaweza kupunguza hatari ya maafa yanayosababishwa na upepo mkali.
Katika jitihada za kudhibiti athari za hali ya hewa, Malenya ameagiza Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wilayani Namtumbo kusambaza miti na kuhakikisha inatiliwa mkazo katika upandaji wake ili kupunguza madhara kama yaliyojitokeza kutokana na upepo mkali.
Hata hivyo Mkuue huyo wa wilaya amewahakikishia waathirika kuwa serikali inaendelea kutafuta njia za kuwasaidia waliopata madhara.
Malenya amesisitiza umuhimu wa kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti ili kuimarisha hali ya hewa. na kupunguza uharibifu wa makazi unaotokana na mabadiliko ya tabianchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.