MAAFISA Ugani 10 wa Mkoa wa Ruvuma wamepatiwa mafunzo ya Upimaji wa Afya ya Udongo.
Mafunzo hayo yametolewa na Wataalam kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Mkuu wa Mafunzo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Frenk Mabagala katika mafunzo hayo amesema mambo yanayosababisha afya ya udongo kupungua ikiwemo kulima kwa mda mrefu bila kutumia mbolea,Kutumia Mbolea bila kupima afya ya udongo,Mmomonyoko wa wa udongo pamoja na kilimo cha kuchoma Moto.
Mabagala ameeleza umuhimu wa kupima udongo katika mafunzo hayo ikiwemo matumizi sahihi ya Mbolea,Udongo uliokufa huzalisha bila kuleta tija kwa mkulima.
“Ili kurudisha uhai au afya ya udongo mkulima anahitaji kuongeza virutubisho mbalimbali muhimu kwa mmea pampja na kiasi cha virutubisho vinavyohitajika katika udongo wa shamba lake”.
Hata hivyo Mabagala ameelezea kuwa afya ya udongo kupimwa katika maabara zilizojengwa (TARI MLINGANO),Ukiriguru,Selian,Uyole,SUA,Kipimo cha haraka rapitest kit ,maabara za Mkononi na maabara zinazotembezwa kwa gari.
Kwa upande wake Mtafiti George Kingumbi amesema upungufu wa potassium katika udongo huondoa virutubisho vinavyotembea katika mimea viashiria kuanza kuonekana katika majani ya chini kukauka kwenye kingo za jani.
Kingumbi amesema chachu ya udongo (Soil PH) huathiri upatikanaji wa wa Virutubisho kwa kubadirisha muundo kirutubisho kwenye udongo,kuboresha chachu ya udongo kwa kiwango kinachopendekezwa kunaweza kuongeza upatikanaji wa virutubisho muhimu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Januari 27,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.