• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

UPUNGUFU wa mbolea Songea kubakia historia

Imewekwa kuanzia tarehe: November 10th, 2023

 Upungufu wa mbolea mkoani Ruvuma na nchi nzima kwa ujumla utabaki historia baada ya kiwanda cha mbolea cha ITRACOM kuzalisha mbolea inayokidhi mahitaji ya mbolea ya wakulima kwa mwaka.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa Kiwanda cha ITRACOM FERTILIZER LIMITED Dkt Keneth Masuki wakati anazungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa ghala la mbolea la kiwanda hicho mtaa wa Msamala Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Dkt Masuki amesema kiwanda hicho cha mbolea ambacho kimejengwa mkoani Dodoma kina uwezo wa kuzalisha mbolea na virekebishi vya udongo zaidi ya tani milioni 1.5 kwa mwaka hivyo kukidhi mahitaji ya mbolea katika nchi nzima ambayo ni kati ya tani 600,000 hadi 700,000 kwa mwaka.

“Uwekezaji wa kiwanda hiki ni wa kimkakati kwa sababu Mheshimiwa Rais alipokuwa Makamu wa Rais ndiye aliyeanza hizi harakati za uwekezaji wa kiwanda,mchakato ulianza mwaka 2020,uwekezaji ni mkubwa kwa kuwa kiwanda ni kikubwa ambacho kinailetea heshima Tanzania’’,alisisitiza Masuki.

Ameongeza kuwa katika Bara la Afrika hakuna kiwanda kikubwa cha mbolea kama hicho ambacho kinatengeneza mbolea iliyochanganywa mbolea za chumvi chumvi na samadi ambapo amesema kiwanda kimetokana na Mwekezaji ambaye alikuwa na kiwanda kama hicho nchini Burundi.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa ghala la kiwanda cha ITRAFOM,mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye aliwakilishwa na Mheshimiwa Kapenjama Ndile amesema matokeo ya kiwanda hicho ni jitihada za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye alifanya juhudi za kumshawishi Mwekezaji ili kuhakikisha kiwanda cha mbolea kinaanzishwa nchini kukidhi mahitaji ya  wakulima.

Amesisitiza kuwa kufunguliwa kwa ghala hilo mjini Songea ni fursa ya kiwanda hicho kifungua maghala mengine mengi ya mbolea maeneo ya vijijini waliko wakulima wengi.

“Nimeambiwa ITRAFOM inatengeneza aina tatu za mbolea ambazo ni  mbolea ya kupandia(FOMI PANDIA),mbolea za kukuzia (FOMI KUZIA) na mbolea za kuzalisha (FOMI NENEPESHA)  ni matumaini yangu kuwa wakulima watajengewa uwezo kuhusu namna ya kutumia mbolea hii ili uzalishaji uwe na tija’’,alisisitiza.

Amebainisha kuwa katika msimu wa mwaka 2022/2023 wakulima mkoani Ruvuma wamezalisha tani 1,870,800 ya mazao ya chakula,biashara na mbogamboga na saw ana asilimia 95 ya lengo la mavuno ya tani 1.965,072 .

Hata hivyo amebainisha kuwa kwa mazao ya chakula pekee katika kipindi hicho zilivunwa tani 1,598,163 na mazao ya biashara zilivunwa jumla ya tani 94,741.

Amesisitiza kuwa uzalishaji mkubwa wa mazao katika mkoa wa Ruvuma ulitokana na matumizi makubwa ya mbolea ambapo katika msimu wa mwaka 2022/2023 Mkoa ulitumia zaidi ya tani 71,000 na kwamba katika msimu huu wa mwaka 2023/2024 hadi sasa tani zaidi ya 41,000 za mbolea zimesambazwa kwa wakulima.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.