Manufaa ya ushirika katika Mkoa wa Ruvuma,yanajionesha bayana kutokana na Mkoa huo kutegemea sekta ya kilimo kama nguzo kuu ya uchumi na ndiyo iliyowaweka wananchi hususani wakulima pamoja na kufanya kazi kwa umoja kama jamii moja.
Ushirika katika Mkoa wa Ruvuma umewasaidia wakulima kufanya shughuli za kilimo bila kuteteleka licha ya kukutana na changamoto kadhaa ikiwemo kukomesha mifumo holela ya ununuzi wa mazao ambayo imechangia kuwarudisha nyuma wakulima na wana ushirika kwa ujumla.
Mifumo holela ya ununuzi wa mazao kabla ya serikali ya awamu ya sita ilitumiwa na wafanyabiashara wanaonunua mazao kuwanyanyasa wakulima kwa kuwalipa malipo kidogo wakati wa mauzo na kuwafanya wasinufaike na mazao yao na hatimaye baadhi yao kukata tamaa na kuachana na shughuli za kilimo.
Miongoni mwa Vyama vikuu vya Ushirika vilivyopata mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni Chama Kikuu cha Ushirika wa Mazao mchanganyiko ya Kilimo wilayani Tunduru(TAMCU LTD).
Hapa Kaimu Meneja wa TAMCU Marcelino Mrope anasema,tangu Rais Dkt Samia aingie madarakani wamepata mafanikio lukuki ikiwemo kuimarika kwa kilimo cha mazao ya kimkakati hasa mazao yanayouzwa kwa mfumo wa stakabadhi gharani ambayo ni korosho,mbaazi na ufuta yanayolimwa kwa wingi katika wilaya hiyo.
Mrope anataja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni pamoja na ongozeko kubwa la Viuatilifu vinavyotolewa bure kwa asilimia mia moja kwa wakulima wa zao la korosho Mkoa wa Ruvuma wanaohudumia na TAMCU.
Anaeleza kuwa,katika kipindi hiki kumekuwa na ongezeko la zaidi ya asilimia 200 ya upatikanaji wa viuatilifu kwa ajili ya zao la korosho, ambapo viuatilifu vyote vilivyotolewa vilitolewa bure kwa asilimia mia moja na Serikali.
Anasema,katika katika kipindi cha miaka mitatu wamepokea zaidi ya lita 322,542 za Salfa ya maji kati ya hizo lita 11,680 wamepokea msimu wa kilimo 2021/2022,lita 131,310 msimu wa 2022/2023 na msimu 2023/2024 wameshapokea zaidi ya lita 179,552.
Kuhusu upatikanaji wa Salfa ya unga anasema,katika kipindi cha miaka mitatu serikali imepeleka zaidi ya Kilogram milioni 7,417,125 wilayani Tunduru,ambapo Kilo 528,000 zimepelekwa katika msimu wa kilimo 2021/2022,kilo 1,555,725 msimu wa kilimo 2022/2023 na kilo 5,333,400 kwa msimu wa kilimo 2023/2024.
Anasema,wakati Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani mwaka 2021 uzalishaji wa korosho ulikuwa chini ya tani 15,000,lakini kwa muda wa muda mitatu wa Uongozi wake wakulima wa korosho Mkoani Ruvuma wanaosimamiwa na Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru(TAMCU)waliongeza uzalishaji kutoka tani 15,000 hadi kufikia tani 25,284,50 na wastani wa bei ni Sh. 1,996.16.
Mrope anaeleza kuwa,katika msimu 2022/2023 wakulima walizalisha kilo milioni 15,218,006 na bei ilikuwa Sh.1,706.00 na msimu uliopita wa 2023/2024 zaidi ya kilo 26,062,323 zilizalishwa na kuuzwa kwa wastani wa bei ya Sh.1,746.00 kwa kilo moja na pamoja na kupata mabomba elfu moja mia nane sitini na saba (1,867) ya kupulizia korosho ambayo yamepatikana kwa ruzuku ya asilimia 50.
Anasema,katika kipindi hiki tatizo la upatikanaji wa Vifungashio (gunia za kuhifadhia korosho) halipo kwa maana upatikanaji wake ni mkubwa na rahisi sana hadi kuwa na bakaa ya gunia tupu laki moja sitini na tatu mia sita thelasini na tano (163,635) yenye uwezo wa kuhifadhi kilogramu za korosho milioni kumi na tatu na tisini elfu mia nane (13,090,800).
Anasema,katika msimu wa kilimo 2021/2022 gunia zilizopelekwa kwa wakulima ni 190,625,msimu 2022/2023 zilikuwa 300,000 na msimu 2023/2024 gunia 439,000 hivyo kufanya jumla ya gunia 929,625 zilifika kwa ajili ua kuhifadhi korosho.
Anasema, kabla ya uongozi wa awamu ya sita kuingia madarakani hali ya upatikanaji wa vifungashio ilikuwa ya kusuasua ambayo ilichangia sana msimu wa mauzo ya korosho kuchukua muda mrefu na hivyo kuchelewesha mauzo ya korosho zinazokusanywa kutoka kwa wakulima.
Mrope aneleza kuwa,Katika kipindi cha miaka mitatu 2021 hadi 2024, mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na kuwa na soko la uhakika kwa mazao yanayouzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.
Anatoa mfano kwa zao la Mbaazi ambalo limeimarika na kuendelea kuuzwa chini ya mfumo wa Stakabadhi za Gharani na imepelekea hata mikoa jirani kama Lindi na Mtwara nayo kuanza kuuza zao hilo kwenye mfumo wa stakabadhi gharani na hali hiyo imewafanya wakulima kuachana na soko holela ambalo halina tija kwao hasa baada ya kuwepo kwa soko la uhakika nchini India.
Kwa upande wa zao la mbaazi anasema,bei imeimarika kwani katika msimu ulioisha wa 2023/2024 bei wastani ilikuwa shilingi elfu mbili na nane(2,008) kwa kilo moja kutoka Sh.200 kabla ya serikali ya awamu ya sita kuingia madarakani.
Kwa mujibu wa Mrope katika kipindi cha miaka mitatu wakulima walifanikiwa kuzalisha na kuuza jumla ya kilo milioni 12,176,398 zenye thamani ya Sh.bilioni 17,970,584,380.19 kati ya hizo kilo milioni 4,111,845 zenye thamani ya Sh.bilioni 5,235,425,002.00 zilizalishwa katika msimu wa 2021/2022 huku bei ya wastani ikiwa ni Sh. 1,273.25 kwa kilo moja.
Katika msimu wa mwaka 2022/2023 wilaya ya Tunduru ilizalisha jumla ya kilo milioni 3,035,692 zenye thamani ya Sh.bilioni 2,633,233,690.00 ambapo bei ya wastani ilikuwa Sh.898.25 na msimu 2023/2024 jumla ya kilo milioni 5,028,861 zenye thamani ya Sh.bilioni 10,101,925,688.19 zilizalishwa na bei ilikuwa Sh. 2008.97 kwa kilo moja.
Naye Mwenyekiti wa Tamcu Mussa Manjaule anasema,kuimarika kwa bei ya mazao yanayouzwa kupitia mfumo wa stakabadhi gharani,umesaidia hata bei ya zao la ufuta kuimarika.
Manjaule anasema,katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya sita uelekeo unaonesha bei kuongezeka mwaka hadi mwaka kutoka Sh. 2,94.44 mwaka 2021/2022 hadi kufika Sh. 3,684.54 msimu 2023/2024 ambapo kilo milioni 9,569,095 zimezalishwa na kuwaingizia wakulima jumla ya Sh.bilioni 13,025,984,329.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.