• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

USHIRIKISHWAJI vijana mradi jengo la Halmashauri Mbinga,ulivyomfurahisha RC IBUGE

Imewekwa kuanzia tarehe: June 15th, 2021

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Mbinga kuwashirikisha vijana katika mradi wa ujenzi ofisi za Halmashauri hiyo unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni mbili.

RC Ibuge ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea mradi wa jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo unaotekelezwa katika eneo la Kiamili Kata ya Mkako wilayani Mbinga.

R.C Ibuge ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo unaojengwa na SUMA JKT,ambapo amepongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mtendaji,Juma Mnwele.

Brigedia Jenerali Ibuge ameridhishwa na jitihada zinazofanywa  kuwezesha jamii kupitia vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ikiwemo kikundi cha vijana cha Chipukizi ambacho kinajishughulisha na ufyatuaji wa tofali zinazotumika kwenye ujenzi wa jengo hilo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Juma Mnwele akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo,amesema hadi sasa zimeletwa shilingi bilioni moja na zaidi ya shilingi  milioni 400 hadi sasa zimetumika kwa ajili ya hatua za awali za utekelezaji wa mradi huo ikiwemo ununuzi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi.

“Tumemkabidhi mradi SUMA JKT kuanzia Juni 2 mwaka huu,kwa kuanzia tumemlipa shilingi milioni 78,tunaridhika na utekelezaji wa mradi huu,vijana wameshirikishwa kikamilifu katika mradi huu’’,alisema Mnwele.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Mbinga amesema Kikundi cha Chipukizi kilichopo Kata ya Kigonsera mwaka huu 2021 kimenufaika kwa kupatiwa mkopo wa shilingi Milioni 22.

Amesema kikundi hicho ambacho kinashiriki kwenye mradi huo,ni miongoni kwa vikundi vingine zaidi ya 20 ambavyo vimewezeshwa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 330 ikiwa ni asilimia 10 ya fedha za mapato ya ndani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa mwaka wa fedha 2020/2021hadi 2021/2022.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Juni 15,2021

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.