Mkoa wa Ruvuma unajiandaa kwa tamasha kubwa la “Usiku wa Mwanamke,” linalotarajiwa kufanyika tarehe 9 Machi 2025 katika Ukumbi wa Bombambili.
Hafla hii inalenga kusherehekea mafanikio ya wanawake na kuhamasisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.
Kwa mujibu wa waandaaji, tukio hili litaanza saa 1:00 usiku na litahusisha burudani, muziki wa live band, vinywaji, chakula, na fursa za kufanikisha mahusiano ya kijamii na kibiashara (networking).
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Mariam Nyoka, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma.
Kaulimbiu ya usiku huo ni “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji.”
Viingilio kwa hafla hiyo vimetangazwa kuwa Tsh 50,000 kwa VIP na Tsh 30,000 kwa daraja la kawaida. Washiriki wanatakiwa kufuata mavazi rasmi yenye rangi nyeusi (Dress Code: Black).
Hafla hii inatarajiwa kuleta pamoja wanawake kutoka sekta mbalimbali ili kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo yao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.