Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mh. Stewart Nombo, amewataka wananchi na viongozi katika Vijiji na Kata kusimamia ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, ili fedha hizo ziweze kusaidia katika ukamilishaji wa miradi ya maendeleo.
Ameyasema hayo jana, wakati akiongea na wananchi katika ziara ya Siku moja iliyofanyika, Tarafa ya Mpepo katika Kata za Mpepo, Liparamba,Tingi Lumeme na Kingerikiti , Akiwa na Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi, wakati Akitembelea na akikagua Miradi Mbalimbali ya Maendeleo.
Mh. Nombo amefafanua kuwa, Halmashauri kwa sasa tunatakiwa kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato, ili tuweze kujitegemea kwa kuwa na mapato yatakayoweza kusaidia ukamilishaji wa miradi mbali mbali inayoibuliwa na kutekelezwa na wananchi. Tukitaka kufanikiwa katika ukusanyaji wa Mapato, lazima tushirikiane kati ya Wananchi, Viongozi na Wataalamu kwa Ujumla kwa kuwa wakusanyaji wa mapato wanakusanya katika Ngazi za Vijiji.
Amewataka Watendaji wa Vijiji na Kata kusimamia Ukusanyaji wa Mapato, kwa kuziba mianya inayosababisha kupotea mapato katika Vituo (mageiti) ya Ukusanyaji mapato na Kutoa Taarifa kwa wakusanyaji wasio waaminifu, ili mapato yatakayopatikana yatumike kukamilisha miundombinu ya miradi mbalimbali itakayowanufaisha wananchi katika Maeneo yao.
“Nichukue fursa hii kuwakumbusha wananchi na viongozi kuwa kila mtu kwa nafasi yake ahakikishe anasimamia ukusanyaji wa mapato na kuwasimamia wakusanyaji mapato, haturuhusu kuwapo kwa upotevu wa mapato kwa maslahi yao binafsi hivyo maafisa watendaji wa vijiji na kata wahakikishe watoza ushuru wanafanya kazi kwa uaminifu, ili fedha zote tuzipeleke kwenye miradi ya Maendeleo”
Aidha amewapongeza wananchi wa Tarafa ya Mpepo kwa kushiriki kikamilifu kuchangia Miradi ya Maendeleo, na kuwa eleza kuwa katika kipindi cha uongozi wake atahakikisha fedha zote za Miradi ya Maendeleo zinatumika vizuri na wananchi wote wajitoe kuchangia maendeleo.
Kamati ya fedha na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imetembelea jumla ya miradi 12 yenye thamani ya TZS. 607,975,644.91 ya Afya na Elimu ,na kuridhishwa na mwenendo ya miradi hiyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.