Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya Boost, Lanis pamoja na Swash katika Halmashauri ya Wilaya Songea ambapo Serikali imetoa Zaidi ya Shilingi bilioni 1.1 ya utekelezwaji wa miradi hiyo
Kanali Thomas amewataka na kuwahimiza Wananchi kulinda miradi yote ya maendeleo ambayo Serikali imetoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo, hivyo ni wajibu wao kuilinda na kusimamia ili kuunga mkono juhudi za Serikali ambapo pia amewataka viongozi katika ngazi zote kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo .
Ziara hiyo ameianza leo Juni 27, 2023 kwa kukagua miradi Boost pamoja na Swash katika kata Parangu, Peramiho na Mpitimbi “B” katika Halmashauri ya Wilaya Songea pia anatarajia kuendelea na ziara hiyo katika Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.