Maafisa kutoka Kitengo cha Ustawi wa Jamii, Idara ya Maendeleo ya Jamii na Dawati la Jinsia na Watoto watoa elimu ya jinsia, haki za mtoto pamoja na makatazo ya kisheria kwa watoto. Wanafunzi kutoka shule tatu za sekondari zilizopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru walipokea elimu hii. Shule hizo ni Shule ya Sekondari Matemanga, Shule ya Sekondari Kiuma, na Shule ya Sekondari Namwinyu.
Juhudi hizi zililenga kuwalinda na kuwaelimisha wanafunzi kuhusu masuala muhimu ya jinsia na haki zao. Mtaalamu kutoka Jeshi la Polisi, Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto, Koplo Humphrey, alitoa elimu kuhusu jinsia na makatazo ya kisheria kwa wanafunzi. Elimu hii ililenga kuwajengea uelewa wanafunzi kuhusu masuala ya kijinsia na kuwasaidia kutambua na kuzuia aina zote za ukatili na unyanyasaji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.