IKulingana na ripoti ya utafiti wa mwaka 2011,asilimia 15 ya aina za samaki wa maji baridi duniani wanapatikana ziwa Nyasa ambapo kuna aina ya samaki tofauti zaidi ya 600,huku kukiwa aina ya samaki wa mapambo zaidi ya 400.
Ndani ya ziwa Nyasa kuna viumbe wengine ambao hawapatikani katika ziwa lolote duniani wanapatikana katika maeneo tofauti ndani ya ziwa Nyasa kutegemeana na aina na usalama wa maisha yao.
Jonathan Ruanda Mtaalam wa kuzamia samaki wa mapambo katika ziwa Nyasa na Mfanyabiashara wa samaki hao anasema tangu mwaka 1960 samaki hai wa mapambo walianza kuuzwa katika nchi za Ulaya na Marekani.
Hata hivyo anasema nchi nyingi kama vile Japani, Sweden, Uturuki, Denmark, Canada, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani zilivutiwa na samaki wa mapambo kutoka ziwa Nyasa kutokana na kuwa na sifa ya kipekee yaani rangi nzuri za kupendeza na hakuna sehemu nyingine wanapatikana samaki wa mapambo wa aina hii.
Afisa Maliasili wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe anabainisha kuwa Ziwa Nyasa pia limesheheni utajiri mkubwa wa viumbe hai wakiwemo fisimaji, mamba, nyoka na viboko ambao ni kivutio kikubwa cha utalii.
“Ndege wanaohamia kutoka Ulaya na baadhi ya nchi za Afrika wanapatikana maeneo ya mwambao mwa ziwa Nyasa ambao ni kivutio kikubwa cha utalii.
Ndege hao huja kwa ajili ya kujipatia chakula cha aina mbalimbali katika mwambao wa ziwa Nyasa wakiwa kwenye misafara yao’’,anasisitiza Challe.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.