• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

UTEKELEZAJI wa ilani ya CCM miaka mitano mkoani Ruvuma katika sekta ya elimu

Imewekwa kuanzia tarehe: July 19th, 2020

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme anatoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya miaka mitano kuanzia mwaka 2015 hadi 2020

SEKTA YA ELIMU

  • Maelekezo ya Ilani ya CCM ya Uchaguzi ya mwaka 2015 katika sekta ya Elimu ni kuhakikisha elimu katika ngazi zote inakuwa na ubora unaostahili ili kuwezesha vijana na makundi mengine kumudu ushindani wa soko la ajira ambalo wigo wake umepanuka ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Msisitizo mkubwa wa Serikali ni kuendelea kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.
  •  
  • Hali ya utoaji wa Elimu, taaluma Na miundombinu ya shule katika Mkoa 
  • Katika kutekeleza maelekezo ya Ilani, Mkoa umefanya jitihada mbalimbali katika kuboresha sekta ya elimu kwenye ngazi zote.
  • UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI TANGU 2015-2020

Idadi ya Shule; Tangu mwaka 2015 hadi 2020 Mkoa umekuwa na ongezeko la idadi ya shule za msingi 103 kutoka  idadi ya shule 670 zilizokuwepo  mwaka 2015 hadi shule  773 mwaka 2020. Shule za sekondari zimeongezeka kutoka idadi ya shule 111 mwaka 2015 hadi shule 205 kufikia mwaka 2020 sawa na asilimia 54 ambalo ni ongezeko la shule 94.

Uandikishaji wa  wanafunzi umeongezeka na kuimarika ambapo kuna ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa idadi ya wanafunzi  50021  hadi kufikia Juni 2020 ukilinganisha na idadi ya wanafunzi 47978  mwaka 2015 sawa na  ongezeko la asilmia 4.2 .

Mafanikio ya uandikishaji na mahudhurio ya wanafunzi yameimarika  pia kwa upande wa elimu ya Sekondari ambapo hadi Juni 2020 kuna wanafunzi 74,613 ukilinganisha na wanafunzi 55,643 waliokuwa shuleni mwaka 2015. Ongezeko hili ni la wanafunzi 18,970  sawa na asilimia 75.

Mafanikio haya yametokana na Mpango wa Utoaji wa Elimu Bure unaowezeshwa na Serikali ya awamu ya tano ya Mhe, Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ikiwa ni pamoja na;

  • Kuongezeka kwa miundombinu ya vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, Mabweni, vyoo, mabwalo na maabara.
  • Ununuzi wa vifaa vya kujifunza na kufundishia hususani vitabu vya ziada na kiada kwa wanafunzi ambavyo vimegawiwa katika shule zote.

Hali ya ufaulu wa mtihani ya Kitaifa; Ufaulu katika mitihani ya darasa  la saba, kidato cha nne na kidato cha sita umeongezeka hadi mwaka 2019 ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2015.

MWAKA
WALIOFAULU
ASILIMIA
MTIHANI
2015
17298
68.4
DARASA LA SABA
2019
26534
83.70
2015
6868
74.58
KIDATO CHA NNE
2019
10226
86.06
2015
1199
81.7
KIDATO CHA SITA
2019
3572
99.72

 

Miundombinu katika Sekta ya Elimu;

Katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Mhe, Rais ametupatia fedha za utekelezaji wa miradi ya sekta ya elimu kiasi cha shilingi 15,328,933,835.29 kuwezesha uwepo wa miundombinu katika Sekta ya Elimu kama inavyoonesha katika jedwali lifuatalo;

ELIMU YA MSINGI

AINA

IDADI YA MIRADI

THAMANI (TSH.)

Ujenzi wa Madarasa mapya
461

4,495,680,244.17

Ukamilishaji wa maboma ya vyumba vya madarasa
67

837,500,000

Ujenzi wa nyumba za walimu
36

543,255,117

Ofisi za walimu
24

172,032,650

Jumla ndogo

6,048,468,011.17

ELIMU YA SEKONDARI

AINA
2015 -2020
Ukarabati wa Shule Kongwe
3

2,882,868,464.65

Ujenzi wa vyumba vya madarasa
235

3,271,798,602.04

Nyumba za walimu
6

180,080,500

Jengo la Utawala
1

50,000,000

Matundu ya vyoo vya wanafunzi
74

194,899,282

Mabweni
14

852,827,000

Ukamilishaji vyumba vya maabara
68

1,847,991,975.43

Ujenzi wa mabwalo ya chakula
6

1.732, 542,833.41

Viti vya wanafunzi
7281

161, 786,300

Meza za wanafunzi
6836

177, 266, 540

JUMLA

9,280,465,824.12






  • Utekelezaji wa Programu ya Elimu Bila Malipo

Mhe. Rais amekuwa akiupatia Mkoa fedha kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Elimu Bila Malipo tangu mwaka 2015 ambapo jumla ya Tshs.  26,707,325,111.30 zimepokelewa kwa muda wa miaka mitano hadi kufikia mwaka 2020.

  • Utekelezaji wa Mpango huu umeleta mafanikio katika kuongeza kiwango cha uandikishaji kwa wanafunzi wa darasa la awali, la kwanza na kidato cha kwanza pamoja na kuimarisha usimamizi wa uboreshaji wa Elimu katika ngazi ya shule na kata ikiwemo kuimarisha taaluma na kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika mitihani.

Tunaendelea kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt.John Pombe Joseph Magufuli kwa kuanzisha Mpango huu wa elimu bure kwa watanzania.

Vituo vya Ufundi Stadi na VETA

Katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Mhe, Rais ameboresha eneo la mafunzo ya ufundi stadi ambapo kwa Mkoa sasa kuna vyuo 3 vya VETA hadi mwaka 2020 kutoka chuo 1 mwaka 2015. Hii ni baada ya kuletewa fedha za ujenzi wa vyuo 2 vya VETA vya Nyasa na Namtumbo ambapo chuo cha VETA Namtumbo kimegharimu Tsh. biln. 4. Na VETA Nyasa Tsh. 2,196,581,105.29 na hivyo ufanya jumla ya fedha iliyotumika kuwa shilingi  6,196,581,105.29

Vyuo vya Ualimu na Elimu ya Juu

Vyuo vya Ualimu

Mkoa una vyuo vya ualimu 3 vinavyotoa mafunzo ya ualimu. Kati ya hivyo chuo cha ualimu Songea ni cha Serikali na 2 ambavyo ni chuo cha ualimu Kiuma na Chuo cha Ualimu Nazaleti vinamilikiwa na mashirika binafsi.

Ili kuweka mazingira bora ya kufundisha na kujifunzia katika kipindi cha  miaka mitano Mhe, Rais ametuletea fedha kwa ajili ya ukarabati wa chuo cha ualimu Songea kwa thamani ya fedha shilingi 1,485,760,357.26.

 

Elimu ya Juu

Mkoa kwa kushirikiana na Serikali, wadau wa maendeleo unaendelea kuhamasisha uwekezaji katika eneo la uanzishaji wa vyuo vya elimu ya juu. Hadi kufikia mwaka 2020 kuna vyuo vya elimu ya juu 3 ukilinganisha na uwepo wa chuo 1 ilipokuwa 2015. Vyuo hivyo ni matawi 2 ya Chuo Kikuu huria cha Tanzania katika wilaya ya Tunduru na Songea. Vyuo vingine ni Tawi la chuo Kiuu Cha Kilimo Sokoine (SUA) kilichopo wilaya ya Tunduru na chuo cha maliasili na Utalii kinachojengwa wilaya ya Nyasa.

  • Miradi inayoendelea

Katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ya miaka mitano jumla ya miradi 2558 yenye thamani ya shilingi 8,525,829,742 inaendelea kutekelezwa katika ujenzi wa miundombinu ya madarasa, vyoo vya wanafunzi, mabweni na  mabwalo kama ilivyoainishwa katika jedwali lifuatalo;

ELIMU YA MSINGI

Madarasa

128

2,560,000,000

Matudu ya vyoo

1107

3,966,229,742

ELIMU YA SEKONDARI

Madarasa

38

760,000,000

Matundu ya vyoo

36

39,600,000

Mabweni

10

800,000,000

Mabwalo

4

400,000,000

JUMLA

2558

8,525,829,742

 

Shughuli nyingine zilizotekelezwa na mafanikio yaliyopatikana kwa mwaka 2015-2020

  • Katika kuimarisha usimamizi na ufatiliaji wa shughuli za elimu Mkoa ulipokea magari 4 kutoka kwa Mhe. Rais kwa ajili ya Ofisi ya Elimu Mkoa, Chuo cha Ualimu Songea na Ofisi 2 za uthibiti ubora kwa Halmashauri za Nyasa na Manispaa ya Songea. Vilevile, Mhe. Rais ametoa pikipiki 175 kwa Maafisa Elimu Kata kwa lengo la kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa elimu katika ngazi ya kata, jambo ambalo limewaondelea changamoto ya usafiri.
  • Serikali imeimarisha mazingira ya utendaji ya Wathibiti Ubora wa Elimu kwa kujenga ofisi 5 zenye jumla ya thamani ya shilingi 760,162,500/= katika halmashauri za wilaya za Tunduru, Songea, Mbinga, Nyasa na Manispaa ya Songea.

Mafanikio haya yanayoonekana wazi kwa kipindi cha miaka mitano katika sekta ya elimu yametokana na utashi mkubwa alionao Mhe. Rais katika kuwaletea maendeleo watanzania kupitia sekta ya elimu.

ITAENDELEA KATIKA SEKTA YA AFYA

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.