Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, imesema ni jukumu lao kuhakikisha wanawaunga mkono na kuwasemea mema wabunge wa Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini kwa kutumia majukwaa yote muhimu.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Tunduru, Komred Hussein Mkuwia, amesema jumuiya hiyo itahakikisha inawalinda wabunge hao na viongozi wa chama kwa namna yoyote ile ili wabaki salama. Kauli hiyo aliitoa Februari 12, 2025, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Kijiwe cha Kahawa kupitia Selous FM.
Mkuwia amewakumbusha vijana wa Tunduru kujikita kwenye shughuli za kilimo badala ya kukaa vijiweni, akisisitiza kuwa wilaya hiyo ina fursa nyingi, ikiwemo kilimo na uchimbaji wa madini.
Pia amewaomba vijana waendelee kumuunga mkono Mheshimiwa Rais kwa juhudi zake za kuleta maendeleo katika majimbo yote mawili ya Tunduru.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.