UBORESHAJI wa Uwanja wa Ndege wa Songea, mkoani Ruvuma umeleta mabadiliko makubwa katika sekta ya usafiri wa anga na maendeleo ya kiuchumi katika Mkoa wa Ruvuma.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitumia Shilingi bilioni 40.87 kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa uwanja huo.
Kazi zilizofanyika ni pamoja na Urefushaji wa barabara ya kuruka na kutua ndege (runway) kutoka mita 1,625 hadi mita 1,860, na upana kutoka mita 23 hadi 30.na Ujenzi wa maegesho mapya ya ndege (apron) yenye uwezo wa kuhudumia ndege nne aina ya Q400 Bombardier na ndege ndogo tatu kwa wakati mmoja.
Kazi nyingine zilizofanyika ni ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege (control tower) na barabara ya kiungio (taxiway).na Usimikaji wa taa za kuongozea ndege na ununuzi wa gari la zimamoto.
Uboreshaji huu umeufanya uwanja huo kufikia kiwango cha 3C kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) .
Tangu kukamilika kwa mradi huu, idadi ya abiria wanaotumia uwanja huo imeongezeka kutoka 3,900 mwaka 2021 hadi 19,620 mwaka 2024. Hii imesababisha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuongeza safari zake hadi mara tatu kwa wiki .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, alikagua na kuridhishwa na maendeleo ya uwanja huo wakati wa ziara yake mkoani Ruvuma mnamo Septemba 23, 2024. Alisisitiza kuwa uwanja huo sasa ni kitovu muhimu cha biashara na maendeleo katika kanda ya kusini .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.