• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

UZALISHAJI wa mazao Ruvuma wafikia tani milioni 1.8

Imewekwa kuanzia tarehe: May 23rd, 2024


UZALISHAJI wa mazao mkoani Ruvuma umeongezeka kutoka tani 1,623,509.57 msimu wa mwaka 2020/2021 hadi  kufikia tani 1,823,509.57  katika msimu wa mwaka 2022/2023.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema kuongeza kwa uzalishaji wa mazao hayo kumechangiwa na wakulima kuongeza matumizi ya mbolea ya ruzuku ambayo imeweza kuwafikia wananchi katika maeneo yao kwa gharama nafuu.

Amebainisha kuwa kutokana na serikali kuweka ruzuku kwenye mbolea. matumizi ya Mbolea yameongezeka kutoka tani 50,524.50 msimu wa 2021/2022 hadi tani 93,955.7 msimu wa 2023/2024.

“Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kufanya maboresho makubwa katika Sekta ya Kilimo kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya kilimo, mifumo ya ruzuku ya pembejeo na vyombo vya usafiri kwa Maafisa Ugani’’,alisisitiza Kanali Abbas.

Amesema Serikali imetoa pikipiki 281 kwa maafisa ugani wote wa Kata na Vijiji kwa kwa Mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuwawezesha Maafisa Ugani kuwafikia wakulima  ili kutoa huduma za ugani kwa wakulima.

Ameongeza kuwa serikali pia imetoa mashine saba za kupima afya ya udongo na kwamba Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo kupitia Taasisi yake ya TARI Uyole na Kampuni ya OCP iliwezesha upimaji wa Afya ya Udongo katika vijiji 100 vya Mkoa wa Ruvuma.

Ameongeza kuwa serikali imejenga maghala 31 yenye uwezo wa kuhifadhi tani 1,000 kila moja katika Halmashauri za Madaba ambako yamejengwa maghala 11, Halmashauri ya wilaya ya Songea maghala 12 na  Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo yamejengwa maghala manane kupitia program ya ujenzi wa maghala kwenye maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya nafaka.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.