Uzalishaji wa zao la parachichi katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma umepaa kwa asilimia 400 katika kipindi cha miaka mitatu.
Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bw. Enock Ndunguru amesema uzalishaji wa zao hilo umeongezeka mpaka kufikia tani 40 katika msimu wa mavuno wa mwaka 2023 ambayo ni sawa na ongezeko la tani 32 ikilinganishwa na tani nane zilizozalishwa mwaka 2021.
Amesema ongezeko hilo limechangiwa na mazingira rafiki yaliyotengenezwa na serikali kwa lengo la kuvutia wakulima kujikita zaidi katika kilimo cha parachichi.
“Eneo la uzalishaji wa zao la parachichi katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga limeongezeka kutoka hekari 80 mwaka 2021 hadi kufikia hekari 182 za sasa, hii inatia moyo kwa hakika”, alisisitiza Ndunguru.
Amesema zao la parachichi licha ya kuwa chanzo cha kipato, lakini pia parachichi ni zao rafiki wa mazingira.
Parachichi, kitaalamu linaitwa Persea Americana ni tunda lenye virutubisho muhimu sana vinavyohitajika katika mwili wa binadamu na linaongeza kipato kwa familia na Taifa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.