NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga, amewataka vijana hususani wasichana kuongeza juhudi katika kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Ametoa rai hiyo wakati akitoa hotuba katika kilele cha wiki ya vijana kilichofanyika katika uwanja wa Majimaji mjini Songea kuelekea maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ambayo yatafanyika Disemba Mosi, mkoani Ruvuma.
"Ninawasihi vijana wote nchini hususani wasichana kuongeza juhudi katika kujikinga na maambukizi ya VVU, Kwa mlioko shuleni na vyuoni wekeni mkazo katika Elimu na kujiepusha na tabia zote hatarishi zinazopelekea kupata maambukizi ya VVU," alisema Mhe.Ummy.
Amewashauru vijana kushiriki katika michezo mbalimbali ili kuimarisha afya na kupata ajira kupitia michezo hiyo na kujiondoa kwenye mazingira hatarishi ya kupata VVU.
Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana wanaoishi na VVU, Pudensiana Mbwiliza, amesema kama vijana wanaunga mkono dira ya Taifa na dunia ya kufikia kizazi kisicho na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI, vifo 0 na unyanyapaa 0 ifikapo mwaka 2030.
Amebainisha kuwa takwimu za utafiti wa viashiria vya UKIMWI Tanzania (THIS) kwa mwaka 2022/23 zimeonyesha kwa kiasi kikubwa jinsi maambukizi ya VVU yanavyoendelea kuwakabili vijana hasa wenye umri wa miaka 15-24 huku kundi kubwa zaidi likiwa ni wasichana.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.