VIJANA sita tu kati ya 240 walioteuliwa na Serikali kupitia Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma mwaka 2024 kwenda kujiunga na chuo cha Ufundi Nazareth kilichopo Mbesa wilayani humo ndiyo walioripoti hadi kufikia Julai 31 mwaka huu.
Vijana walioteuliwa kwa mwaka wa masomo uliopita 2023 katika Chuo hicho walikuwa 114, lakini wanaoendelea hadi sasa na mafunzo ya ufundi ni vijana 8 tu huku wengine 106 hawajulikana walipo.
Serikali kupitia Halmashauri ya wilaya Tunduru iliteua wanafunzi waliohitimu darasa la saba na kidato cha nne mwaka 2023 na 2024 ili kujiunga kwenye mafunzo ya ufundi ili waweze kupata ujuzi katika fani mbalimbali zitakazo wawezesha kupata ujuzi ambao utawasaidia katika maisha yao.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa chuo hicho Ezekiel Mapunda,wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50 ya chuo cha Nazareth Mbesa kinachomilikiwa na Wamisionari wa Kanisa la Bibilia Duniani.
Mapunda amesema,chuo cha Ufundi Nazareth Mbesa kilianzishwa kwa lengo la kuwapa vijana wa Kitanzania elimu ya ufundi ili waweze kujitegemea katika maisha yao na kwamba wakati chuo kinaanzishwa mwaka 1974 walianza na fani ya Useremala na ilipofika mwaka 1976 waliongeza fani ya magari na mwaka 1994 walianzisha fani nyingine za uchongaji na ukelezaji vyuma na uchomeaji.
Kwa mujibu wa Mapunda,ilipofika mwaka 2017 fani mbili mpya za umeme wa majumbani,ushonaji nguo na mapambo zilisajiriwa ili kupanua wigo zaidi kwa watoto wa kike kujiunga na chuo ili nao waweze kujitegemea mara watakapomaliza mafunzo yanayochukua miaka mitatu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa pili wa Shirika la misaada la Makanisa ya Bibilia Duniani Klaus Brinkmann,amewataka Wanafunzi wa chuo hicho kutumia ujuzi na elimu wanayoipata kufikiria kwenda kujitegemea kwa kujiajiri badala ya kuwaza kuajiriwa Serikalini.
Katika risala ya wahitimu iliyosomwa na Selestine Kalo,wameshauri chuo kuleta vifaa vya kisasa kwa ajili ya kufundishia na kujifunzia kutokana na kukua kwa teknolojia hasa uwepo wa magari yanayotumia gesi.Zaidi ya wanafunzi 1000 wamehitimu mafunzo ya fani mbalimbali tangu chou hicho kilipoanzishwa mwaka 1974.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.