Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, amesema kutokana na takwimu zinazotolewa inaonekana kundi kubwa lililoathirika na maambukizi ya VVU ni la vijana.
Ameyasema hayo wakati akifunga mdahalo wa vijana na viongozi wa dini na kimila kuelekea maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ambayo kitaifa itafanyika mkoani Ruvuma.
"Ni Imani yangu kila kijana ana ndoto na ili kufikia ndoto hiyo ni lazima kujiwekea malengo katika kufikia ndoto zako, ili kutokuwa na kikwazo katika ndoto yako ni muhimu kuijua hali yako ya kiafya," alisema Kanali Ahmed
Ameongeza kuwa wanapozungumzia vijana wanazungumzia asilimia 68 ya nguvu kazi ya Taifa na dhahiri hakuna namna wanaweza kufanya shughuli za maendeleo pasipo kutambua nafasi ya vijana ndani ya jamii na kufahamu vipaumbele vyao ikiwemo afya nzuri.
Kanali Ahmed amebainisha kuwa vijana wote kote nchini wameshafahamu kuhusu VVU ingawa wapo vijana wachache wasiojua kwa kina na hawajui namna ya kujikinga hivyo anaamini Elimu ya kwenda kujikinga iliyotolewa kupitia kongamano hilo ni sahihi.
Naye katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, amesema Elimu iliyotolewa kupitia viongozi wa dini na kimila ni ya muhimu kwa vijana katika kukabiliana na janga la UKIMWI.
Ameongeza kuwa adhma kubwa ya Serikali na wadau ni kuelekea mwaka 2030 bila ya kuwa na changamoto ya UKIMWI na inawezekana iwapo mafunzo yaliyotolewa yatatumika kujielimiaha na kuwaelimisha wengine.
Kutokana na takwimu zinazotolewa imeonekana kundi kubwa linaloathirika na lipo hatarini kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ni la vijana.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.