Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, amewataka vijana kuishi kwa kufuata misingi ya dini na utamaduni huku wakikabiliana na changamoto mbalimbali.
Bi. Mary alitoa wito huo wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama kufungua mdahalo wa vijana na viongozi wa dini na kimila uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bombambili mjini Songea kuelekea maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ambayo kitaifa itafanyika mkoani Ruvuma.
Bi. Mary amesitiza umuhimu wa vijana kutumia fursa hiyo kujifunza namna bora ya kujikinga na VVU na kuishi kwa kuzingatia maadili ya dini na tamaduni za Kitanzania.
“Rai yetu kama Serikali ni kuwa vijana kutumia fursa hii kujifunza namna bora ya kukabiliana na kujikinga na VVU, kuishi kwa kuzingatia maadili ya dini na tamaduni zetu, ndio maana kuna viongozi wa dini pia viongozi wa kimila, turejee katika misingi iliyotukuza na kutulea.” alisema Bi. Mary.
Bi. Mary pia alibainisha kuwa mdahalo huo utakuwa chachu ya kuhamasisha jamii katika ngazi ya familia kujitokeza kupiga vita unyanyapaa ili watu wajitokeze kupima na kuwa wafuasi wazuri wa dawa na chanjo zinazotolewa bila malipo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.