Naibu Waziri wa Nishati Mheshimiwa Judith Kapinga amezindua mradi wa umeme katika shule ya Sekondari ya Nyasa mjini Mbambabay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Nyasa, katika Kata ya Chiwanda amesema amelazimika kufanya ziara mkoani Ruvuma, baada ya kuona Wilaya ya Nyasa na Mbinga miradi ya umeme wa REA, haijakamilika katika ngazi ya vijiji.
Amemuagiza Mkandarasi wa REA kukamilisha haraka miradi hiyo Ili serikali ianze kutekeleza miradi ya umeme katika ngazi ya vitongoji.
Aidha amesema katika Wilaya ya Nyasa huduma ya umeme tayari imefika katika vijiji 84.
Kwa upande wao wananchi wa wilaya ya Nyasa wameipongeza Serikali kwa kutatua changamoto ya Umeme katika Kata ya Chiwanda ambayo ipo mpakani mwa Nchi ya Tanzania na Msumbiji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.